NAFASI YA KAZI YA MKURUGENZI WA KITUO CHA HUDUMA YA MTOTO - KKKT-DKMZV / COMPASSION


Uongozi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria (KKKT-DKMZV) Usharika wa Ebenezer Kanisa Kuu Shinyanga kwa Ushirika wenza na Compassion International Tanzania (CIT) unatangaza nafasi moja ya kazi kama kiambatanisho kinavyoeleza. 


NAFASI YA KAZI INAYOTANGAZWA 
Mkurugenzi wa Kituo cha huduma ya mtoto Tz. 236. (Project Director). Nafasi moja. Mkurugenzi wa Kituo cha Huduma ya Mtoto atahusika moja kwa moja katika kamati ya Huduma ya Mtoto ya Ufadhili, kwenye mambo yote yahusuyo Utumishi wa Watendakazi wengine kwa mujibu wa Program Field Manual (PFM) na Huduma ya Mtoto kiujumla ya Compassion International Tanzania katika Ushirikawenza na Makanisa ya Kiinjili Tanzania.

SIFA ZA MWOMBAJI. 
ELIMU
Diploma na kuendelea (kutoka kwenye chuo kinachotambulika/kukubalika na Serikali)

Taaluma katika maeneo ya uongozi/utawala, usimamizi wa biashara, maendeleo ya jamii, maendeleo ya watoto, theolojia na ualimu.

UJUZI/UFAHAMU/SIFA NYINGINE: 
  • Awe ni Mkristo mwaminifu aliyeokoka na mwenye maisha ya ushuhuda kwa maisha yake ya kila siku. 
  • Awe na ufahamu kuhusu mambo ya watoto na maendelo yao, Maendeleo ya jamii, usimamizi wa Miradi, Uhamasishaji wa rasimali jamii, Uongozi wa Kanisa, ualimu 
  • Uwezo wa kutumika katika jamii masikini iliyo katika mazingira hatarishi.
  • Mwenye moyo wa kuwapenda watoto, kufanya kazi za Kanisa na mpenda maendeleo.
  • Mwenye uwezo wa kuongea, kusoma na kuandika lugha ya kingereza kwa ufasaha.
  • Umri kuanzia miaka 25 na si zaidi ya miaka 40 (Kibali maalumu chaweza kufikiriwa kutolewa kwa atakayezidi umri).
  • Asiwe amewahi kutiwa hatiani kwa kosa la jinai au la unyanyasaji wa mtoto.
  • Awe na uwezo na elimu ya kutumia kompyuta (word, excel, Outlook, power point na Internet). 
WAJIBU WA MKURUGENZI WA KITUO.
Kazi muhimu na wajibu wa mkurugenzi wa huduma ya mtoto ni kama ifuatavyo:
  • Kuandaa mpango na bajeti ya Huduma ya Mtoto kwa kushirikiana na watendakazi wengine wa Huduma ya Mtoto na kuwasilisha kwa kamati ya Huduma ya Mtoto kwa uthibitisho na kuidhinishwa na uongozi wa Kanisa 
  • Kutekeleza mpango na bajeti ya programu kama ilivyothibitishwa na kuidhinishwa. 
  • Kusimamia na kuratibu shughuli zote za wafanyakazi wengine wa Kituo cha Huduma ya Mtoto. 
  • Kuwasilisha ripoti kwa kamati, uongozi wa kanisa na huduma ya Compassion International Tanzania kama itakavyo takiwa kwa pande zote husika. 
  • Kuhakikisha kuwa taarifa zote za fedha na watoto zinatunzwa vizuri na kuboreshwa kila mara zinapohitajika. 
  • Kusimamia Maono, Vithaminisho vyote vya Msingi vya Huduma, na Misingi ya Huduma wakati wote wa Uhai wa kituo cha Huduma ya Mtoto. 
  • Kushiriki katika zoezi la usaili wa kuwapata Watendakazi wengine wote wa Kituo cha Huduma ya Mtoto kwa kutoa maoni yake binafsi kuhusu nafasi hizo. 
  • Kuhakikisha mazingira ya Watoto/Vijana kituoni ni salama kwao kujifunza na kushiriki katika program zote za kituo. 
  • Atasimamia na kuwa mwangalizi mkuu wa utekelezaji wa mitaala yote inayotumika kituoni, msimamizi wa shughuli zote za ufundishwaji na usimamizi wa waalimu wote. 
  • Atawajibika kuandaa na kuandika maandiko mbalimbali (Proposals) kwa ajili ya mahitaji mbalimbali ya watoto, wazazi, na kituo kwa ujumla. 
  • Kuhakikisha uwepo wa miundo mbinu inayohitajika kwa watoto/vijana kujifunza kituoni inapatikana kwa njia ya uhamasishaji wa rasilimali zilizopo na kutafuta njia mbadala za kupata miundo mbinu kwa ajili ya watoto/Vijana. 
  • Kuhakikisha ripoti zote za kituo zinazohusu maeneo mbalimbali ya utendaji wa Watendakazi wengine zinaandaliwa na kuwasilishwa kwa wakati na ubora unaotakiwa/unaotegemewa 
  • Kutathmini maendeleo ya watendakazi wengine wa Huduma ya Mtoto na kuwasilisha maoni yake kwa kamati ya Huduma ya Mtoto. 
  • Kufuatilia kwa karibu maendeleo ya kiroho, kielimu, kijamii, kiafya na masuala mengine kwa watoto walio katika programu na kuyachukulia hatua haraka pale inapobidi, pamoja na kuwatembelea majumbani mwao. 
  • Atawajibika kwa matokeo yote tarajiwa, KRIs (Key Result Indicators), matokeo ya ukaguzi, kulingana na PFM. 
  • Kuhakikisha kwamba watoto wameandika barua kwa wafadhili wao kwa wakati muafaka, kiwango/viwango vinavyotakiwa na kwa mujibu wa programu. 
  • Kuhakikisha zawadi za watoto zilizotumwa na wafadhili zinawafikia walengwa kwa wakati muafaka na kwa kiwango kinachopaswa. 
  • Kushiriki katika mafunzo ya kiroho yaliyoandaliwa na huduma ya Compassion International Tanzania katika Huduma ya Mtoto au Huduma ya Mtoto yeyote kwa ujumla. 
  • Kupitisha gharama zote za malipo sambamba na maelekezo yaliyotolewa na kamati ya Huduma ya Mtoto na pia kulingana na miongozo ya kifedha ya Compassion International. 
  • Kuwasaidia watendakazi wengine wa Huduma ya Mtoto na kushirikishana wajibu wao pale wanapohitaji. 
  • Kuwatembelea watoto majumbani na mashuleni mwao sambamba na mpango na programu ya Huduma ya Mtoto. 
  • Kutoa taarifa kwa kamati ya Huduma ya Mtoto, mchungaji kiongozi na katika ofisi za huduma ya Compassion International Tanzania juu ya ubadhirifu wa fedha au tabia mbaya kwa mmojawapo wa wafanyakazi wengine wa Huduma ya Mtoto inapojitokeza. 
  • Kushiriki katika shughuli zote za barua za watoto zinazoingia na zinazotoka kwenda kwa wafadhili. 
  • Atahitajika kutunza kitabu cha hundi na kitabu cha hati ya malipo. 
  • Kuhakikisha wakati wote kwamba watoto walioandikishwa katika Huduma ya Mtoto kwa ajili ya ufadhili ni wale tu wanaokidhi masharti yaliyowekwa na Compassion International Tanzania. 
  • Kuwatia moyo wazazi na walezi wa watoto na wajumbe wa kanisa kuwasaidia watoto kukua kiroho na kuwa na maendeleo mazuri katika masomo. 
  • Kuhusika katika majukumu mengine yoyote yaliyotolewa na kamati ya Huduma ya Mtoto au ofisi ya huduma ya Compassion International Tanzania. 
  • Atatoa kila wiki taarifa ya maandishi kwa Mchungaji kiongozi juu ya utendaji na maendeleo ya kituo. 
  • Katika utendaji wake wote wa majukumu/wajibu atawajibika kwa kamati na Mchungaji kiongozi/Katibu wa Usharika 
  • Atahakikisha kunakuwa na ibada ya asubuhi ya watendakazi wote kabla ya kuanza kazi na kushiriki kikamilifu. 
  • Ataitisha na kuratibu vikao vya wazazi kwa kushirikiana na mwenyekiti wa kamati ya wazazi. 
  • Ataitisha na kuendesha vikao vya watendakazi (staff meeting) mara mbili kwa mwezi au zaidi pale itakapobidi. 
  • Atatafsiri barua zote za watoto zinazotoka kwa wafadhili. 
  • Atasimimamia na kuratibu shughuli zote za wa mama wa ufadhili wa upendo (Esther Encounter) 
  • Atafanya kazi nyinginezo za kiofisi kama atakavyopangiwa na kamati ya kituo cha huduma ya mtoto na uongozi wa kanisa. 
NAMNA YA KUTUMA MAOMBI
Waombaji wenye sifa watume maombi yao kwa:-
Mchungaji Kiongozi,
KKKT- DKMZV Usharika wa Ebenezer Kanisa Kuu.
S.L.P 372,
SHINYANGA.

(Aione Katibu wa Usharika).
AU
KWA BARUA PEPE.
ebenezer.dkmzv@yahoo.com
ibrahimlyanga@yahoo.com 

MAELEKEZO MUHIMU.
Barua iandikkwe kwa lugha ya kingereza, 
Iambatanishwe na:-
  • Fomu ya taarifa binafsi za mwombaji (Curriculum vitae (CV)) ya Mwombaji 
  • Vyeti vya Elimu na Taaluma ya mwombaji pamoja na 
  • Barua ya Utambulisho toka kwa Mchungaji wa Kanisa unaloabudu. 
Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 18/06/2017 saa 16:00.
Tarehe ya Usaili mwombaji atajulishwa (Only shortlisted). 

LIMETOLEWA NA 
KATIBU WA USHARIKA.
KKKT DKMZV USHARIKA WA EBENEEZER KANISA KUU
TEL: +255(0) 282 763 878
Mobile Phones.
+255789991155
+255755754589
+255712 791 818
Email:- ibrahimlyanga@yahoo.com
P. O. Box 372,

SHINYANGA - TANZANIA

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527