KIONGOZI MWINGINE WA CCM AUAWA KWA KUPIGWA RISASI KIBITI

Mwenyekiti wa CCM tawi la Njia nne Iddy Kirungi liliopo katika kijiji cha Muyuyu kata ya Mtunda wilayani Kibiti ameuawa kwa kupigwa risasi akiwa kwake.


Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Kibiti Juma Njwayo,ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Rufiji amethibitisha kutokea mauaji hayo.


Amesema marehemu alipigwa risasi akiwa kwake wakati akijaribu kukimbia.


Njwayo amesema kabla ya kuuawa kwa mwenyekiti huyo, pia wauaji hao walianza kumjeruhi kwa kumpiga risasi ya tumboni mtoto wa marehemu aliyetajwa kwa jina la Nurdin Iddy Kirungi.


Mganga wa zamu katika kituo cha afya Ikwiriri, Dk Rashid Omar alisema walimpokea Nurdin akiwa na jeraha kubwa tumboni mwake ambalo halikutokeza upande wa pili.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527