Monday, May 8, 2017

MAJENEZA HAYA YA WANAFUNZI ARUSHA YAMLIZA RAIS MAGUFULI


Rais Dkt Magufuli ameshindwa kujizuia na kusema kuwa amekumbwa na majonzi makubwa baada ya kuona majeneza 35 ya wanafunzi wa Shule ya Lucky Vicent ya jijini Arusha waliofariki katika ajali ya basi wilayani Karatu Mkoani Arusha.Rais Magufuli ameyasema hayo wakati miili ya wanafunzi 32, walimu 2 na dereva mmoja ikiagwa katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini Arusha na kisha kusafirishwa maeneo mbalimbali kwa ajili ya maziko.


Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Rais Dkt Magufuli aliandika, “Nimepatwa na uchungu na majonzi makubwa ninapoyaona majeneza ya watoto na walezi wao waliopoteza maisha katika ajali ya basi huko Arusha .”


“Tumewapoteza mashujaa wetu ktk elimu. Tuwaombee na tuendelee kuwa na subira, uvumilivu na ustahimilivu 2/2.”


Aidha, Rais Dkt Magufuli amewasihi wa Tanzania kuendelea kuwa wamoja wakati wakiomboleza tukio hili kubwa lililoikumba nchi na kuacha simanzi miongoni mwa watu wengi.


“Tunapoomboleza vifo vya wapendwa wetu tuendelee kuwa wamoja. Mungu ibariki Tanzania.”

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde1 blog Inapatikana Play Store…Download HAPA ,Tuwe Tunakutumia Habari Kwenye Simu Yako
 Bofya Hapa
Share:

Tafuta Habari Hapa

Subscribe You Tube Channel Yetu

 Bofya Hapa

Pakua Videozetu App

Kutana Able wa Michoro

Manju Matemba - Beni

Manju Polosho Myogela

Habari Kuu

TAZAMA HAPA VIDEO 100 ZA NGOMA ZA ASILI ...ANGALIA KAMA UTAONA KABILA LAKO

Habari za leo mpenzi msomaji wa Malunde1 blog hususani wewe mfuatiliaji wa nyimbo za asili..Leo nimeamua kukuletea  nyimbo zaidi ya 100 za ...

Classic Visual Shinyanga

Habari Gumzo Mtandaoni

Mshana Computer Solution

Habari Zilizopita

Jiunge Nasi Hapa

Translate This Blog

Copyright © MALUNDE 1 BLOG | Powered by Malunde