Ajali Tena!! MABASI YA ALLY'S STAR NA ISANZU YAGONGANA USO KWA USO SAMUYE SHINYANGA,ANGALIA PICHA HAPA


Wimbi la ajali limezidi kujitokeza nchini Tanzania ambapo leo Jumanne May 9,2017 basi la Ally's Star lenye namba za usajili T402 ATV likisafiri kutoka Mwanza kwenda Kaliua  Tabora limegongana uso kwa uso na basi la Isanzu T797 DDW lililokuwa likitoka Kahama kwenda Mwanza.


Ajali hiyo imetokea leo majira ya saa mbili asubuhi katika eneo la Samuye barabara ya Shinyanga kwenda Mwanza.

Inaelezwa kuwa chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi wa  dereva wa basi la Ally's Star aliyekuwa anajaribu kulipita gari aina ya Scania T784 BMT lililokuwa limeharibika pembezoni kwa barabara,ndipo akagongana na basi la Isanzu.

Hakuna mtu aliyepoteza maisha katika ajali hiyo lakini abiria 35 katika magari yote mawili wamejeruhiwa na wamekimbizwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga.

Basi la Ally's likijaribu kulipita gari aina ya Scania T784 BMT lililokuwa limeharibika pembezoni kwa barabara
Magari yakiwa yamegongana
Dereva wa basi la Isanzu akiwa amebanwa ndani ya gari na inaelezwa kuwa hali yake ni mbaya
Magari yakiwa yamegongana
Mabasi yakiwa yamegongana
Majeruhi wakipatiwa matibabu hospitali ya mkoa wa Shinyanga

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527