Picha : ADHIMISHO LA MISA YA JUMAPILI KANISA KUU LA MAMA MWENYE HURUMA NGOKOLO- SHINYANGA,TAS YATOA ELIMU MASUALA YA UALBINO


Chama cha watu wenye Ualbino nchini Tanzania (TAS) kimeendelea na kampeni yake ya kutoa elimu kuhusu masuala ya ualbino kwenye mikusanyiko ya watu ambapo leo Jumapili Aprili 2,2017 kimetoa elimu hiyo katika kanisa kuu la Mama Mwenye Huruma la Ngokolo mjini Shinyanga.

Elimu hiyo imetolewa na Afisa Mahusiano na Habari kutoka TAS Josephat Torner wakati wa adhimisho la misa ya pili ya Jumapili ya 5 ya Kwaresma ambayo ilihudhuriwa na mamia ya waumini wa kanisa hilo.

Akizungumza kanisani hapo,Torner aliwataka waumini wa kanisa hilo kuungana na wadau wote wa haki za binadamu katika kupiga vita ukatili wanaofanyiwa watu wenye ualbino.

“Vitendo vya mauaji ya watu wenye ualbino vilianza mwaka 2007,leo mwaka 2017 ni muongo mmoja sasa lakini matukio yanazidi kujitokeza kutokana na tamaa ya mali na madaraka kwa baadhi ya watu,ndiyo maana tumeamua kutoa elimu kuhusu masuala ya ualbino ili watu waache vitendo hivi ambavyo ni chukizo kwa mwenyezi mungu”,alisema Torner.

“Matukio ya kuuawa kwa watu wenye ualbino,kukatwa viungo vyao na sasa makaburi kufukuliwa ni matukio yaliyotufanya tuvunje ukimya,tunaomba viongozi wa dini,waumini na watu wenye mapenzi mema muungane nasi katika vita hii ambayo hatumjui hasa nani ni adui yetu”,alieleza Torner.

Torner aliendelea kutilia mkazo kwa serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na rais John Pombe Magufuli kuongeza nguvu katika mapambano dhidi ukatili wanaofanyiwa watu wenye ualbino.

Akitoa mahubiri wakati wa misa ya Jumapili Paroko Msaidizi kanisa kuu la Mama Mwenye Huruma Ngokolo Padre Pastory Masunga aliwaomba waumini wa kanisa hilo na jamii kwa ujumla kuepuka kuishi kwa kutenda dhambi na kuwataka kumwamini mungu.

“Watu wanadiriki kuua vikongwe,watu wenye ualbino,kula rushwa,kutoa mimba,kufanya ukatili kwenye familia zao,kuwa na chuki na visasi kutokana na kukosa hofu ya mungu,naomba tubadilike,kila mmoja wetu aishi kwa kumtendea haki mwenzake”,alisema Padre Masunga.

Mwandishi Mkuu wa Malunde1 blog,Kadama Malunde alikuwepo wakati wa Misa ya Pili ya Jumapili ya 5 ya Kwarema…Ametuletea picha 27 za matukio…Tazama hapa chini

Kanisa kuu la Mama Mwenye Huruma Ngokolo mjini Shinyanga
Paroko Msaidizi kanisa kuu la Mama Mwenye Huruma Ngokolo Padre Pastory Masunga akitoa mahubiri wakati wa misa ya pili ya Jumapili ya tano ya Kwarema katika kanisa kuu la Mama Mwenye Huruma Ngokolo mjini Shinyanga leo Aprili 2,2017
Waumini wakifuatilia mahubiri kanisani
Paroko Msaidizi kanisa kuu la Mama Mwenye Huruma Ngokolo Padre Pastory Masunga akiendelea kutoa mahubiri kanisani
Waumini wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea kanisani.Wa pili kutoka kulia ni Afisa Mahusiano na Habari kutoka TAS Josephat Torner
Misa ya Jumapili ya 5 ya Kwaresma ikiendelea
Waumini wa kanisa katoliki wakiwa kanisani
Waumini wakiwa kanisani
Misa inaendelea
Afisa Mahusiano na Habari kutoka Chama cha watu wenye ualbino nchini Tanzania (TAS) Josephat Torner akitoa elimu kwa viongozi na waumini wa kanisa katoliki waliohudhuria misa ya Jumapili
Afisa Mahusiano na Habari kutoka Chama cha watu wenye ualbino nchini Tanzania (TAS) Josephat Torner  akizungumza kanisani
Afisa Mahusiano na Habari kutoka Chama cha watu wenye ualbino nchini Tanzania (TAS) Josephat Torner akitoa elimu kuhusu masuala ya ualbino kanisani
Afisa Mahusiano na Habari kutoka Chama cha watu wenye ualbino nchini Tanzania (TAS) Josephat Torner  akiendelea kutoa elimu kuhusu masuala ya ualbino
Waumini wakimsikiliza Josephat Torner
Afisa Mahusiano na Habari kutoka Chama cha watu wenye ualbino nchini Tanzania (TAS) Josephat Torner akizungumza kanisani ambapo aliwataka viongozi na waumini wa kanisa hilo kuungana nao katika vita dhidi ya ukatili kwa watu wenye ualbino
Afisa Mahusiano na Habari kutoka Chama cha watu wenye ualbino nchini Tanzania (TAS) Josephat Torner akizungumza kanisani

Waumini wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea kanisani

Misa ya Jumapili inaendelea


Misa inaendelea
Misa inaendelea 
Waumini wakiwa wamesimama kanisani
Waumini wakitoka kanisani baada ya Misa kumalizika
Afisa Mahusiano na Habari kutoka Chama cha watu wenye ualbino nchini Tanzania (TAS) Josephat Torner akitoka kanisani
Muonekano wa kanisa kuu la Mama Mwenye Huruma Ngokolo Mjini Shinyanga
Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527