MFANYABIASHARA MAARUFU WA MADINI ARUSHA KIZIMBANI KWA KUMPIGA CHUPA MKEWE WAKISULUHISHWA NA BABA MKWE


Mfanya biashara maarufu wa madini jijini Arusha, Venance Moshi
(30)amefikishwa Mahakamani na kusomewa maelezo ya awali katika kesi inayomkabili ya kunshambulia na kumjeruhi mkewe kwa chupa usoni ,wakiwa wanasuluhishwa na baba mkwe, mgogoro wa ndoa yao.

Mbele ya hakimu , Devota Msofe wa mahakama ya wilaya Arusha ,mwendesha mashtaka wa serikali ,Agnes Hyera alieleza mahakama hiyo kuwa mnamo Machi 11 mwaka 2016 katika maeneo ya Moshono kwenye usuluhishi wa mgogoro wa
ndoa yao ,mshtakiwa alinyanyua glasi na kumpiga kwenye jicho la kulia mlalamikaji (mkewe) Agnes Joseph (30)iliyomjeruhi vibaya .

Mwendesha mashtaka aliieleza mahakama hiyo kuwa hatua hiyo ilimsabishia mlalamikaji atokwe na damu nyingi na baadae kutoa taarifa kituo cha polisi ambapo mtuhumiwa alitiwa mbaroni na baadaye kufikishwa mahakamani.

Baada ya kusomewa maelezo hayo mshitakiwa huyo alikana mashtaka ,na hakimu Msofe alipanga siku ya kuanza kusikilizwa kwa shauri hilo,baada ya upande wa jamhuri kudai kuwa wapo tayari kwa usikilizwaji wa kesi hiyo.

Katika shauri hilo la jinai namba 438 la mwaka 2016 ,upande wa jamhuri unatarajia kuwasilisha mashahidi watatu na vielelezo kadhaa ikiwemo hati ya polisi(PF3) , hati ya daktari pamoja na picha za jeraha.

Kesi hiyo imepangwa kusikilizwa February 6 ,mwaka huu ,saa tatu asubuhi.

Aidha katika hatua nyingine ,shahidi namba moja wa kesi hiyo ,Agnes Joseph anatarajia kufungua kesi nyingine ya kudai talaka kwa mumewe huyo waliyefunga naye ndoa mwaka 2012 baada ya ndoa yao kukumbwa na migogoro ya mara kwa mara huku akiambulia kipigo na vitisho.

Alisema ameishi na mumewe huyo katika mazingira ya migogoro na wamekuwa wakisuluhishwa mara kadhaa bila mafanikio.
Na Woinde-Shizza-Arusha

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527