LOWASSA AFUNGUKA KUHUSU WALIOMTABIRIA KIFO

Waziri Mkuu aliyejiuzuru Edward Lowassa, amesema kuwa Serikali ya Chama cha Mapinduzi (CCM), ina watu wenye roho mbaya kwani waliwahi kumuombea kifo,lakini hadi leo anadunda.

Lowassa ambaye alikuwa mgombea urais wa Chadema na kuungwa mkono na vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi(Ukawa), amesema baadhi ya waliomwombea kifo leo hawapo duniani,kwani mungu ndiye anayepanga maisha ya mwanadamu.

“Kule kwa wenzetu kuna watu wenye roho mbaya,kwani hata mimi waliniombea kifo,waliniombea kifo muda mrefu kweli lakini mpaka sasa bado nadunda tu wakati baadhi ya walioniombea hivyo,leo hawapo duniani kwa mapenzi ya mungu”alisema Lowassa.

Lowassa aliyasema hayo jana baada ya wananchi waliokuwa kwenye mkutano wa ufunguzi wa uchaguzi mdogo wa udiwani kata ya Matevezi jimbo la Arumeru Magharibi,kupaza sauti wakimuuliza juu ya hatima ya mbunge wao Lema ambaye yupo Gereza la kisongo kwa miezi miwili sasa.

Katika hatua nyingine, Lowassa aliwataka timu ya kampeni na wananchi kuhakikisha kura haziibiwi kwa kile alichoeleza kuwa Chadema ina nguvu.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527