VIFAA VYA KUANDIKISHA VITAMBULISHO VYA TAIFA - NIDA VYAIBIWA KISHAPU-SHINYANGA



Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga Muliro Jumanne Muliro

****

Vifaa vinavyotumika katika zoezi la kuandikisha vitambulisho vya taifa (NIDA) vimeibiwa na watu wasiojulikana katika jengo la ofisi ya halmashauri ya wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga.




Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Muliro Jumanne Muliro alisema vifaa hivyo vimebainika kupotea leo asubuhi Oktoba 10,2016 katika jengo la ofisi ya halmashauri ya wilaya ya Kishapu.


Alivitaja vifaa vilivyoibiwa kuwa ni kamera mbili aina ya Canon na stendi zake zilizokuwa kwenye mashine mbili za BVR zenye namba TZNID 01546 na TZNID 01559 zenye thamani ya Shilingi 6,000,000/= mali ya shirika la NIDA.


“Afisa kutoka NIDA Sofia Didas Leshabari (30) ,mkazi wa Dar-es-salaam, alibaini kuwa ofisi iliyokuwa inatumika katika zoezi la uandikishaji wa vitambulisho vya taifa kwa watumishi wa umma katika jengo la halmashauri ya wilaya ya kishapu ghorofa ya kwanza chumba namba 46 ilifunguliwa na kuibiwa kamera mbili aina ya Canon na stendi za kamera mbili”,alieleza Kamanda Muliro.

Alisema mbinu iliyotumika kutenda kosa hilo ni kufungua mlango kwa kutumia master key na kwamba upelelezi unafanywa ili wote waliohusika wafikishwe mbele ya mahakama. 

Kamanda Muliro alibainisha kuwa watu waliohusika katika tukio hilo bado hawajafahamika na kwamba watu watatu wanashikiliwa na jeshi la polisi kuhusiana na tukio hilo.


“Vifaa hivi vinatumika kwa zoezi la kuandikisha vitambulisho vya taifa linaloenda sambamba na uhakiki wa watumishi wa umma,vifaa havionekani lakini tunaendelea na uchunguzi juu ya tukio hili ili kujua kama kuna wizi au hakuna wizi wa vifaa”,aliongeza kamanda Muliro.


Mkuu wa wilaya ya Kishapu ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wilayani humo Nyabaganga Talaba alisema ni kweli kamera za NIDA zimepotea na wanaendelea kushirikiana na jeshi la polisi ili kuwabaini wahusika na kupata vifaa hivyo.


Naye mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Kishapu Stephen Magoiga alikiri kupotea kwa kamera mbili na viegesha vyake vilivyokuwa vimehifadhiwa kwenye ofisi ya halmashauri yake kwa ajili ya kupigia picha za NIDA.


Hata hivyo alisema bado hajawapata taarifa zaidi kuhusu upotevu wa vifaa hivyo na kwamba watatoa taarifa kamili baada ya kupata taarifa zaidi juu ya tukio hilo.


TAARIFA YA JESHI LA POLISI KWA VYOMBO VYA   HABARI.

TUKIO LA KUIBWA KWA CAMERA 2 ZAUINDIKISHAJI WA VITAMBULISHO VYA TAIFA (W) KISHAPU.

TAREHE 10.10.2016  SAA 08:00  KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA KISHAPU KATA, NA TARAFA YA KISHAPU ZONE 13 WILAYA YA KISHAPU MKOA WA SHINYANGA SOFIA D/O DIDAS LESHABARI, MIAKA 30, MMASAI, REGISTRATION OFFICER ONE  WA NIDA, MKAZI WA DAR-ES-SALAAM, ALIBAINI KUWA OFISI ILIYOKUWA INATUMIKA KATIKA ZOEZI LA UANDIKISHAJI WA VITAMBULISHO VYA TAIFA KWA WATUMISHI WA UMMA KATIKA JENGO LA HALMASHAURI YA WILAYA YA KISHAPU GHOROFA YA KWANZA CHUMBA NAMBA 46 ILIVUNJWA / FUNGULIWA (TECHNICAL BREAKING) NA KUIBWA KAMERA MBILI AINA YA CANON NA STENDI ZA KAMERA MBILI AMBAZO ZILIKUWA KWENYE MASHINE MBILI ZA BVR ZENYE NAMBA TZNID 01546 NA TZNID 01559 ZENYE THAMANI YA TSH 6,000,000/= MALI YA SHIRIKA LA NIDA . WEZI/ MTU/WATU WALIOHUSIKA  BADO HAWAJAFAHAMIKA.


 MBINU ILIYOTUMIKA KUTENDA KOSA HILO NI KUFUNGUA MLANGO KWA KUTUMIA MASTER KEY. 

UPELELEZI UNAFANYWA ILI WOTE WALIOHUSIKA WAFIKISHWE MBELE YA MAHAKAMA.WATU WATATU WANAHOJIWA / SHIKILIWA NA POLISI KUHUSIANA  NA TUKIO HILO . RPC SHINYANGA.

Na Kadama Malunde- Malunde1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527