Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

WANAOUA KWA KUKODIWA WAUA WANAWAKE WAWILI,MTU NA JIRANI YAKE WAKILA CHAKULA HUKO GEITA

Watu wawili wameuawa kwa  kukatwa katwa   mapanga na watu wanaosadikiwa kuwa wanakodiwa kwa ajili ya kuwakata vikongwe kwa imani za kishirikina  katika mkoa wa Geita.

Tukio hilo limetokea tarehe 20  mwezi huu majira ya  saa mbili usiku katika kijiji cha Hililika kata  ya Bukoli wilayani Geita.

Kaimu Kamanda wa Jeshi la polisi Mkoani Geita Peter Kakamba alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuwataja waliouawa kuwa ni Agness Mihayo (22) na Nyanjige Mtula(65) wote wasukuma na wakazi wa kijijij hicho.

Kamanda Pita aliongeza kuwa Agness ni jirani yake na Nyanjige na siku hiyo Agnes alikwenda kwa Nyanjige kumtembelea kama jirani yake na alipofika alikuta anakula naye alianza kula kabla hawajamaliza kula inasadikika watu wasiofahamika walikuja na kuanza kuwakata mapanga na kuwauwa palepale na kutokomea kusikojulikana.

Alisema uchunguzi wa tukio hilo unaendelea ili kubaini chanzo cha tukio hilo na watuhumiwa wa tukio hilo wanatafutwa na jeshi la polisi  kwa ajili ya kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.

Matukio ya kuwauwa vikongwe kwa imani za kishirikina katika Mkoa wa Geita yanazidi kushamiri huku wananchi wakiomba serikali kuwapa  kanda maalum kama mkoa wa mara huenda matukio ya mauaji yanaweza kupungua.

Na Valence Robert-Malunde1 blog-Geita

TAFADHALI BOFYA HAPA U LIKE PAGE YETU TUKUTUMIE "HABARI" MOJA KWA MOJA KILA ZINAPOTOKEA

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com