TFF, KDFA WAHITIMISHA MAFUNZO YA UKOCHA KAHAMA


wahitimu wa mafunzo ya ukocha (grassroot) wakiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi
Mwenyekiti wa chama cha mpira wa miguu Kahama Salumu Hussein akizungumza wakati wa kuhitimisha mafunzo ya makocha
Mkufunzi wa makocha nchini Raymond Gweba kushoto akiwa na mgeni rasmi Felix Ntibabara

NEEMA NKUMBI HUHESO DIGITAL&HUHESO FM


Jumla ya makocha 35 kutoka mikoa mitatu ya Geita, Tabora na Shinyanga wamehitimu kozi ya awali ya ualimu wa mpira wa miguu Grassroots (kocha) mafunzo yaliyofanyika wilayani Kahama mkoani Shinyanga.

Mafunzo hayo ya siku tano yalianza rasmi Aprili 18 na kuhitimishwa April 22, 2024 yalikuwa yakifundishwa na mkufunzi wa Kozi hiyo nchini Raymond Gweba kutoka shirikisho la soka nchini TFF.


Mgeni rasmi Felix Ntibabara ambaye ni afisa utamaduni, sanaa na michezo Manispaa ya Kahama ameshiriki zoezi la ufungaji kozi hiyo na ugawaji vyeti kwa washiriki wote amewataka washiriki kwenda kuufanyia kazi ujuzi walioupata ili kuibua vipaji kwani wilaya ya Kahama Ina vipaji vingi.


Aidha mwenyekiti wa chama Cha soka wilaya ya Kahama Salum Husein amesema kuwa timu zote ndani ya wilaya ya Kahama zinapaswa kufundishwa na makocha wenye ujuzi wa soka hivyo waliopata kozi hiyo ya Grassroots wakawe walimu wazuri na KDFA itawalinda.


Hata hivyo baadhi wahitimu wa mafunzo hayo Aisa Godson na Hamad Sule wamesema kuwa wamefurahi kupata mafunzo hayo kwani yamewasaidia kubadili mitazamo waliyokuwa nayo katika ufundishaji hivyo watayatumia vyema kuwafundisha watoto mashuleni kuleta chachu ya soka la Kahama

Makocha 31 wametoka wilaya ya Kahama, Geita wawili na Tabora wawili.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post