DC MKUDE ATAKA WATANZANIA KUENDELEA KUUENZI NA KUULINDA MUUNGANO WA TANGANYIKA NA ZANZIBAR VIZAZI NA VIZAZI

Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude akizungumza kwenye Sherehe za Miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar wilayani humo iliyoambatana na Mdahalo pamoja na Dua na Maombi kwa Madhebebu ya Kiislamu na Kikristo.

Na Marco Maduhu,KISHAPU

MKUU wa wilaya Kishapu Joseph Mkude,amewasihi Watanzania kuendelea kuuenzi na kuulinda Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kwa vizazi vyote, ili kuendelea kufurahia Amani, Mshikamano na Umoja ulioachwa na Waasisi wa Muungano huo.

Waasisi wa Muungano ni Hayati Abeid Amani Karume ambaye alikuwa Rais wa kwanza Zanzibar,pamoja na Hayati Julius Kambarage Nyerere alikuwa Rais wa kwanza Tanganyika, ambao waliunganisha nchi hizo mbili kuwa moja tarehe 26/4/ 1964 na kuitwa Tanzania.
Mkude amezungumza hayo leo Aprili 25,2024,ikiwa ni siku moja kabla ya kusherehekea Miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar hapo kesho,kwenye Mdahalo wa Muungano uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu ulioambatana Sambamba na Dua na Maombi kutoka Madhehebu ya Kiislamu na Kikristo.

Amesema Watanzania wanapo Sherehekea miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, hawana budi kuwaenzi viongozi ambao ni Waasisi wa Muungano huo, kwa kuendelea kudumisha Amani,mshikamano,upendo na umoja, ili nchi iendelee kuwa tulivu na kusongambele kimaendeleo.
"Muungano huu wa Tanganyika na Zanzibar umekuwa na faida kwetu, umejenga taifa moja,lenye watu wamoja wanazungumza lugha moja, na hata kufanya kazi na kushika Madaraka kwa nchi zote mbili bila ya ubaguzi, na kufanya biashara bila ya mipaka," amesema Mkude .

Aidha,amesema kupitia Muungano huo hali ya ulinzi na usalama inaendelea kuimarika kwa pande zote mbili, na Amani kuendelea kutawala, huku akiwapongeza Marais wote hadi wa sasa Dk.Samia na Husein Mwinyi kwa kuendelea kuuenzi na kuulinda Muungano.
Nao Wazee wilayani Kishapu akiwamo Alexander Manyesha na Felista Masanja, wamesema Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, amesaidia sana kudumisha Amani ya Tanzania hasa katika suala la ulinzi.

Wamesema Watanzania wanapaswa kuendelea kudumisha Muungano na wasije wakajaribu kuuvuruga, sababu ndiyo Tunu ya Amani, ndiyo maana hadi leo nchi ya Tanzania hakujawahi tokea Vita tangu kupatikane kwa Uhuru.
Kauli Mbiu katika Sherehe za Muungano Mwaka huu 2024 inasema"Miaka 60 ya Muungano wa Tanzania,tumeshikamana,tumeimarika kwa maendeleo ya Taifa letu".

TAZAMA PICHA HAPA CHINI👇👇

Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude akiendelea kuzungumza kwenye Sherehe za miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar wilayani humo.
Mzee Alexander Manyesha akitoa Simulizi Nchi ilivyokuwa kabla ya Muungano na baada ya kuwa na Muungano.
Bibi Felista Masanja akielezea faida ya kuwa na Muungano.
Mzee Edward Sengeti akieleza faida ya kuwa na Muungano.
Sheikh Adamu Njiku kutoka BAKWATA Kishapu akiongoza Dua ya kuombea Amani Taifa na kuendelea kudumisha Muungano.
Mchungaji Patrick Zengo wa Kanisa la KKKT Kishapu akiongoza Maombi ya kuombea Amani Taifa na kuendelea kudumisha Muungano.
Sherehe za miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar pamoja na kufanyika Dua na Maombi zikiendelea wilayani Kishapu.
Seherehe za miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zikiendelea wilayani Kishapu.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post