WANANCHI KISHAPU WAOMBEA AMANI YA TANZANIA MIAKA 60 YA MUUNGANO


Na Sumai Salum - Kishapu

Mkuu wa Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga Joseph Mkude amewasihi wananchi kuendeleza desturi ya kuliombea taifa la Tanzania lidumu na amani,umoja na mshikamano kwa maslahi mapana ya maendeleo.

Dc Mkude ameyasema hayo leo April 22,2024 alipokuwa kweye maombi na dua maalumu ya kuliombea taifa kufuatia maadhimisho ya miaka 60 ya Muungano maombi yaliyokutanisha viongozi na wananchi wa madhehebu yote yaliyofanyika katika viwanja vya SHIRECU wilayani humo.

"Watanzania wenzangu  kipekee nimshukuru Mungu kwa upendo na huruma zake kutupa uzima na kuishi kwenye taifa letu zuri la Tanzania, zaidi sana neema ya kumjua na kutambua amani,umoja mshikamano vinapatikana kwake ndio maana siku hii tumeacha vyote na kuja kumuomba Mungu kwa pamoja katika viwanja hivi ili aendelee kulitunza taifa na viongozi wetu" ,amesema Mkude.

Sanjari na hayo amewasihi vijana pamoja na wafuasi wa vyama mbalimbali vya siasa kuepukana na siasa na maneno ya uchochezi yatakayopelekea kupoteza amani,umoja,upendo na mshikamano kwa wananchi.

Kwa upande wake mwenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Kishapu Jiyenze Seleli amesema Chama Cha Mapinduzi ambacho ni chama tawala wanaheshimu maamuzi ya wananchi ikiwa wamepewa dhamana ya kuongoza nchi hivyo wanaendelea kuhakikisha amani naumoja ulioanzishwa na waasisi Mwalimu Julias Nyerere wa Tanganyika na Sheikh Abeid Amani Karume wa Zanzibar unaendelea na hawako tayari kuona unavurugika kwa utashi wa baadhi ya watu wenye nia ovu.

Hata hivyo sheikh wa tarafa ya Kishapu Adam Njiku aliyemwakilisha sheikh wa wilaya hiyo amesema Mwenyezi Mungu pekee ndiye awezaye kutoa ulinzi licha ya Jeshi kuwepo na viongozi kwa sababu anajua na kitambua moyo wa kila mwanadamu.
 
Baadhi ya Viongozi kutoka madhehebu ya kikristo na kiisilamu wilayani Kishapu mkoani Shinyanga wakiwa kwenye viwanja vya shirecu leo wilayani humo kuliombea taifa la Tanzani amani na umoja kuelekea  miaka 60 ya muungano.
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Joseph Mkude (kushoto) akiwaaga wageni waalikwa kwenye maombi na dua ya kuliombea taifa la Tanzania amani kwendea miaka 60 ya muungano yaliyofanyika kwenye viwanja vya Shirecu wilayani humo hii leo.
Mkuu wa wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga Joseph Mkude akizungumza  kwenye maombi na dua maalumu ya kuliombea taifa la Tanzania amani kuelekea miaka 60 ya muungano yaliyofanyika katika viwanja vya Shirecu wilayani humo
Kushoto ni mchungaji John Daudi Kingu wa kanisa la EAGT Maendeleo Mhunze na kulia ni mkuu wa Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga Joseph Mkude wakiwa kweye maombi maalumu ya kuliombea taifa la Tanzania amani hii leo kuelekea  miaka 60 ya muungano
Mchungaji wa kanisa la EAGT Kishapu mkoani Shinyanga John Duba  akiwakilisha viongozi wa madhehebu ya Kikristo kuliombea Taifa la Tanzania amani na umoja kuelekea maadhimisho ya miaka 60 ya muungano maombi yaliyofanyika  kwenye viwanja vya Shirecu wilayani humo
Sheikh wa tarafa ya Kishapu wilayani Kishapu mkoani Shinyanga Adamu Njiku akisoma dua maalumu ya kuliombea taifa la Tanzania hii leo kwenye viwanja vya Shirecu wilayani humo
Wanakwaya wa kanisa la EAGT Maendeleo Mhunze EMC kwaya wakiimba kwenye maombi na dua kuliombea taifa la Tanzania amani  na umoja kuelekea maadhimisho ya miaka 60 ya mungano maombi hayo yaliyofanyika kweye viwanja vya Shirecu wilayani Kishapu mkoani Shinyanga
Mwenezi Ccm wilaya ya Kishapu Jiyenze Seleli akizungumza  kwenye maombi na dua ya kuliombea taifa la Tanzania amani kwendea miaka 60 ya muungano yaliyofanyika kwenye viwanja vya Shirecu wilayani humo
Kushoto ni katibu wa CCM wilaya ya Kishapu Peter Mashenji na kulia ni Katibu Mwenezi CCM wilaya Jiyenze Seleli wakipiga makofi kuwashangilia wanakwaya ya EMC walivyoimba kwenye maombi na dua ya kuliombea taifa la Tanzania amani kwendea miaka 60 ya muungano yaliyofanyika kwenye viwanja vya Shirecu wilayani humo

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post