
Konstebo Josephat Mtema,Dsm
Leo September 01,2026 katika Ofisi ya Uhamiaji kurasini, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Patrobas Katambi (Mb) amefanya ziara ya Kikazi.
Waziri Katambi alipokelewa na mwenyeji wake Kamishna Jenerali wa Uhamiaji CGI Dkt. Anna Makakala na kuanza Ziara yake kwa kufanya kikao na Makamishna wa uhamiaji kwa kusomewa Ripoti maalumu kutoka Idara ya Uhamiaji Tanzania ripoti Iliyosomwa na CGI Dkt. Makakala.
Katika Ripoti hiyo CGI Dkt. Makakala alimweleza Mhe. Katambi kwamba Idara ya Uhamiaji inamshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuiwezesha Idara katika kuendelea kutekeleza Miradi ya maendelea kwa kujenga Ofisi za uhamiaji kwa ngazi ya Wilaya na makazi ya Watumishi wa Uhamiaji kwa Tanzania Nzima na kufunga mifumo ya utoaji huduma kwa Kidigitali.
Aidha Waziri Katambi alipata Fursa pia ya kutembelea Mifumo mbalimbali iliyowekwa katika ofisi ya Uhamiaji Kurasini ya utoaji huduma na kuzungumza pia na Wananchi na wageni waliofika kupatiwa huduma za kiuhamiaji
"Nimeridhishwa na Utoaji huduma na ripoti iliyosomwa mbele yangu inaonesha jinsi gani Idara ya Uhamiaji Tanzania inafanya kazi zake kiweledi kwa kufata sheria na kanuni za nchi pia haki na wajibu kwa kila mtu niwahase Watumishi wa Uhamiaji kuendelea kutoa huduma bora pasipo upendeleo wowote kwa Mwananchi na wageni wanaofika Tanzania kwani kufanya hivyo kutaleta taswira nzuri kwa Idara yetu ya Uhamiaji" , alisema Waziri Katambi.
Ziara hii ya kikazi ni mwendelezo wa ziara zake katika Taasisi na Idara zilizopo katika wizara ya mambo ya ndani ya nchi pamoja na kukagua Miradi mbalimbali ya maendeleo.

Social Plugin