Na, Elizabeth Cosmas,Shinyanga
Wananchi wa Mkoa wa Shinyanga wametakiwa kuacha kutumia miwani na dawa za macho bila kufanyiwa vipimo na kupata ushauri kutoka kwa wataalamu wa afya ya macho, ili kuepuka madhara yanayoweza kujitokeza kutokana na matumizi yasiyo sahihi.
Ushauri huo umetolewa leo sept 01,2026 na Mratibu wa Huduma za Tiba katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga, Dkt. Alistidi Ngalawa, wakati wa ufunguzi wa kambi ya uchunguzi na matibabu ya magonjwa ya macho inayofanyika katika hospitali hiyo.
Dkt. Ngalawa amesema baadhi ya wananchi wamekuwa na tabia ya kutumia miwani au dawa za macho bila kupata uchunguzi wa kitaalamu, hali inayoweza kuwafanya kutumia huduma zisizoendana na mahitaji yao.
“Tumekuwa tukipokea wagonjwa wa macho wa aina tofauti lakini aslimia kubwa ni kundi watu wa makamo kuanzia umri wa miaka 40 na kuendelee ambalo kundi hili changamoto yake kubwa nauonaji hafifu kutokana na kukua lakini kutokana Jeografia ya mikoa mingi ya kanda zwa kuwepi kwa hali ya hewa ya kiangazi ,na maeneo yenye vumbi sana na hivyo kuplekea wwagonhwa wengi kupata changamoto ya maco kwa asilimia kubwa.
Aidha Dkt,Ngalawa ameongezea kuwa kumekuwa na wimbi kubwa la watu wengi kutumia vifaa vya kujikinga na changamoto ya macho na njia za asili kujitibia na hivyo kutoa rai kwa wananchi wa Mkoa wa Shinyanga kuacha kujichukulia maamuzi ya kutumia njia zozote za kujikinga nakuwaona matabibu wa huduma hizo kupata ushauli wa kitaalamu zaidi
"Nitoe wito kwa wananchi wote kuacha kuamini imani za nje bila kwenda kuwaona wataalamu wanahusika na changamoto zote za macho wananchi wanapaswa kuhakikisha wanapata vipimo na ushauri wa kitaalamu kabla ya kutumia miwani au dawa za macho”
Dkt Paul akitoa wito kwa wananchi kuja kuafanya vipimo katika hosptali hiyo.
Kwa upande wake, Daktari Bingwa wa Macho kutoka Hospitali ya Mkoa wa Simiyu, Dkt. Paul Kabuche, ambaye anaongoza huduma katika kambi hiyo, amesema kuna sababu mbalimbali zinazoweza kuchangia kuongezeka kwa changamoto za afya ya macho, hususani katika maeneo ya Kanda ya Ziwa.
Dkt. Kabuche amesisitiza umuhimu wa wananchi kufanya uchunguzi wa macho mapema ili kubaini matatizo ya uoni na magonjwa mengine ya macho kabla hayajaendelea na kusababisha madhara makubwa.
“Kuna sababu mbalimbali ambazo zinasababisha kuwepo kwa changamoto ya afya ya macho na mpaka sasa katika kambi yetu tumepokea makundi tofauti tofauti ambayo yameathilika na tatizo hili hasa kundi la wazee ambao changamoto yao kubwa ikiwa ni uoanaji hafifu kutokana na kuongezeka kwa umri na hivyo kupelekea kuona kwa shida lakini sababu nyingin kiwa ni pumu ya macho , presha n.k na kutambua changamoto hizo ni kuja kufanya uchunguzi wa kitabibuna niseme tu kuwa wananchi wote Ni muhimu kufanya uchunguzi wa macho ili matatizo ya uoni na magonjwa ya macho yaweze kubainika mapema na kupata matibabu yanayostahili.”
Mwananchi akitoa wito kwa wakazi wote wa Mkoa wa Shinyanga kuja kupata matibabu ya kitaalamu.
Aidha, baadhi ya wananchi waliojitokeza katika kambi hiyo kwa ajili ya uchunguzi na matibabu ya macho wameeleza kufurahishwa na huduma walizopata, huku wakitoa wito kwa wananchi wengine kujitokeza na kutumia fursa hiyo Bertha Yohana mkazi wa Shinyanga ni moja ya wanufaika wa kuwepo kwa kambi hiyo amesema kuwa kuletwa kwa daktari bingwa kumewapa nafasi kuja kufanya uchunguzi wa kina ambapo huduma hiyo imesogezwa ndani Mkoa wao
“Tunawashukuru wataalamu kwa kuona umuhimu wa kuleta huduma hii katika hospitali yetu ya hapa Mwawaza ili kila wananchi mwenye changamoto ya macho apatae nafasi ya kupata matibabu ya kitaalamu zaidi lakini tunashukuru kwa huduma wanazotupatia. Tunawaomba wananchi wengine wajitokeze kwa wingi ili nao waweze kupata huduma na kufahamu hali ya afya ya macho yao.”
Kambi hiyo ya uchunguzi na matibabu ya magonjwa ya macho inaendelea katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga, ambapo wananchi wanapata fursa ya kufanyiwa uchunguzi na kupata huduma za kitaalamu kuhusu afya ya macho.
Lengo ni kuwafikia wananchi wengi zaidi na kuwahamasisha kuchukua hatua mapema pale wanapobaini changamoto za uoni au dalili za magonjwa ya macho.














Social Plugin