Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

VIJANA LINDENI NCHI YENU: KATAMBI


Na Mwandishi wetu, Shinyanga

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Patrobas Katambi amewataka Vijana kuwa wazalendo na kuilinda nchi yao ikiwa ni pamoja na kukataa kutumika kuharibu amani iliyopo nchini.

Waziri katambi ametoa kauli hiyo mkoani Shinyanga akizungumza na kundi la mafundi ujenzi huku akiwaomba kufichua na kufikisha taarifa za uhalifu kwa Mamlaka za Serikali mapema ili kuweza kudhibiti wimbi la watu wenye nia ovu.

“Mkishaingia kwenye vita ya kupigana wenyewe kwa wenyewe kwasababu ya dini,misingi ya ukabila,misingi ya ukanda,mnaanza kugombanishwa kwa misingi ya vyeo,kugombania madaraka ya kisiasa,wanawafadhili baadhi yenu mnapewa fedha mnasema tukinukishe alafu wewe na mimi tunabaki tunateseka,una bibi yako kijijini yeye wakati wa vita atakimbilia wapi?leo hii ukiwa mkimbizi autoitwa fundi tena,heshima utoipata utaitwa mkimbizi kwasababu nchi yenu mmekubali watu waichome kwasababu ya tamaa.”amesema Waziri Katambi

Waziri Katambi amesema Serikali inaheshimu haki za binadamu na inazisimamia na kuzitekeleza kwasababu Tanzania ni nchi inayofuata misingi ya utawala wa sheria.

“Ndugu zangu mafundi kwenye sehemu zenu za kazi huko mnakojenga kuna watu wanakuja endeleeni kutupa taarifa vyombo vya ulinzi na usalama,tupeni taarifa mnazoshuku za kiusalama ili tuijenge nchi yetu,”amesema Waziri Katambi

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com