Kamati ya Sera ya Fedha ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imepandisha kiwango cha Riba yaBenki Kuu (CBR) kutoka asilimia 5.75 hadi asilimia 6.25 katika robo ya tatu ya mwaka inayoanza Julai hadi Septemba 2026.
Akizungumza katika mkutano na viongozi wa benki, taasisi za fedha na waandishi wa habari, Gavana wa BoT ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Sera ya Fedha, Bw. Emmanuel Tutuba, amesema uamuzi huu unalenga kudhibiti ongezeko la mfumuko wa bei unaotokana na kupanda kwa bei za mafuta, mbolea na gharama za usafirishaji, hali inayotokana na mgogoro unaoendelea Mashariki ya Kati.
‘Kamati imeona kuwa ongezeko hili la riba ya Benki Kuu ni sahihi katika kuhakikisha mfumuko wa bei unabaki ndani ya lengo la asilimia 3 hadi 5, na kuendelea kuchangia ukuaji wa shughuliza uchumi.”. Amesema Gavana Tutuba.
Ameongeza kuwa, bei za chakula zinatarajiwa kupungua kufuatia mavuno mazuri ya msimu wakilimo wa mwaka 2025/26. Vilevile, thamani ya shilingi inatarajiwa kuimarika kutokana namapato yatokanayo na mauzo nje ya nchi, ikiwemo dhahabu, mazao ya kilimo, na shughuli za utalii.
“Hali hii itasaidia kupunguza bei za chakula na bidhaa zinazoagizwa kutoka nje ya nchi, nahivyo kuhakikisha mfumuko wa bei unabaki ndani ya lengo katika nusu ya pili ya mwaka 2026”.
Kuhusu mwenendo wa uchumi nchini, Gavana Tutuba amesema uchumi umeendelea kuimarika licha ya changamoto zilizotokana na mgogoro wa Mashariki ya Kati. Tanzania Bara unakadiriwa kukua kwa asilimia 6 katika nusu ya kwanza ya mwaka 2026, ukichangiwa na sekta za kilimo, ujenzi, madini, huduma za kifedha na usafirishaji, huku uchumi wa Zanzibar ukikadiriwa kukua kwa asilimia 6.6 kutokana na kuimarika kwa sekta za utalii na ujenzi.
Aidha, alieleza kuwa mfumuko wa bei kwa Tanzania Bara uliongezeka hadi asilimia 4.2 mwezi Mei 2026 kutoka asilimia 3.2 mwezi Machi, lakini uliendelea kuwa ndani ya lengo la asilimia 3–5, ukisaidiwa na ruzuku ya mafuta iliyotolewa na Serikali mwezi Mei na Juni. Zanzibar, mfumuko wa bei uliongezeka hadi asilimia 5.5 kutoka asilimia 4.9, karibu na lengo la asilimia 5.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Mabenki Tanzania (TBA), Bw. Theobald Sabi, ameipongeza Benki Kuu kwa kusimamia uchumi wa nchi ambao umeendelea kukua licha yauwepo wa migogoro ya kisiasa ulimwenguni.






Social Plugin