Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano, Mhe. Dkt. Evaline Munisi amesema kuwa Mafanikio ya utekelezaji wa Dira 2050 yanategemea Mahusiano mema kwa kuwa ndio matokeo ya Utawala bora, Amani, Usalama na Maendeleo endelevu.
Ameyasema hayo leo Julai 3, 2026 wakati wa kikao na viongozi wa dini kilicholenga kujadili namna ya kuendelea kuimarisha ushirikiano kati ya Serikali na viongozi wa dini katika kutekeleza majukumu ya maendeleo ya Taifa na kukuza ustawi wa wananchi.
Amesema, Serikali inatambua nafasi muhimu ya taasisi za dini katika kujenga jamii yenye maadili, umoja na mshikamano, hivyo amewahimiza viongozi wa dini kuendelea kushirikiana na Serikali katika kuhamasisha wananchi kushiriki kikamilifu katika utekelezaji wa Dira ya Taifa 2050 kwa manufaa ya Taifa na vizazi vya sasa na vijavyo.
“Sote tunatambua umuhimu wa malezi mema kwa Watoto na Vijana, Jamii yenye hofu ya Mungu ina nafasi kubwa ya kuendelea kuishi `kwa amani na utulivu” Amesema Naibu Munisi.
Halikadhalika, Serikali itaendelea kuthamini mchango wa taasisi za dini na kuimarisha ushirikiano unaolenga kuendeleza amani, mshikamano na umoja wa kitaifa kwa ustawi wa Wananchi.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti viongozi wa dini wameiomba serikali kufanya urasimishaji wa somo la dini kuanzia ngazi za chini za elimu ili kujenga maadili mema kwa vijana kuanzia ngazi za msingi




Social Plugin