Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

DC KISHAPU AZINDUA JUKWAA LA UWEZESHAJI WA WANAWAKE KIUCHUMI, AWAKUMBUSHA KUZINGATIA MAADILI

Mkuu wa Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga Mhe. Peter Masindi akizungumza kwenye uzinduzi wa Jukwaa la kuwawezesha wanawake kujikwamua kiuchumi wilayani humo Julai 16, 2026 katika ukumbi wa Kishapu  akiwa ndiye mgeni rasmi

Na Sumai Salum-Kishapu


Mkuu wa Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga, Mhe. Peter Masindi, amezindua rasmi Jukwaa la Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi Wilaya ya Kishapu, akiwataka wanawake kulitumia jukwaa hilo kujikwamua kiuchumi huku wakidumisha maadili, amani na mshikamano katika familia na jamii.


Akizungumza katika uzinduzi huo uliofanyika Julai 16, 2026 katika ukumbi wa Shule ya Sekondari Kishapu, Mhe. Masindi amesema Wanawake ni nguzo muhimu katika maendeleo ya familia, jamii na Taifa, hivyo wanapaswa kutumia jukwaa hilo kujenga uchumi wao bila kusahau majukumu yao ya msingi.

"Mnapaswa kuendelea kutambua kuwa ninyi ni nyenzo muhimu katika familia, uzalishaji na malezi bora. Msijiingize kwenye mikopo isiyo ya lazima inayoweza kuwaletea migogoro na kuwanyima amani katika familia zenu," amesema Mhe. Masindi.

Ameongeza kuwa wanawake wana mchango mkubwa katika maamuzi ya maendeleo na kuwataka wanajukwaa kuhakikisha wanatumia fursa zinazopatikana kujiletea maendeleo endelevu.

Mbunge wa Viti Maalum Vyuo Vikuu ambaye pia Mwenyekiti wa Jukwaa la Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi Mkoa wa Shinyanga, Dkt. Regina Malima, aliwataka wanawake kuhakikisha wanamiliki ardhi, kuwekeza katika shughuli za ujasiriamali na kukuza biashara zitakazowafanya kuwa wafanyabiashara wakubwa ndani na nje ya Wilaya ya Kishapu.

Kwa upande wake, Mbunge wa Jimbo la Kishapu, Mhe. Lucy Mayenga, alisema wanawake ni jeshi kubwa la maendeleo na kwamba wakidumisha amani, umoja, mshikamano na upendo wataendelea kuwa mfano bora katika jamii.

Kwa upande wake, Afisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Shinyanga, Rehema Edson, amesema serikali imeandaa bajeti na mipango ya kazi kwa ajili ya kuendeleza shughuli za jukwaa hilo, huku akiwataka wadau mbalimbali kuendelea kushirikiana katika kuwawezesha wanawake kiuchumi.
Katibu Tawala wilayani Kishapu mkoani Shinyanga Fatma Mohamedi akizungumza kwenye uzunduzi wa Jukwaa la kuwawezesha wanawake kujikwamua kiuchumi wilayani humo Julai 16, 2026 katika ukumbi wa Kishapu huku Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe. Peter Masindi akiwa ndiye mgeni rasmi


Mwakilishi wa Mkuu wa divisheni ya Maendeleo ya Jamii Halamashauri ya Kishapu, Juma Ndoela, akisoma taarifa ya jukwaa hilo, imeeleza kuwa jukwaa la uwezeshaji wanawake kiuchumi ni sehemu ya utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs), hususan lengo namba tano la usawa wa kijinsia na uwezeshaji wa wanawake.


Taarifa hiyo pia imeeleza kuwa jukwaa hilo lilianzishwa rasmi mwaka 2022 na hadi sasa limefanikiwa kuunda majukwaa katika ngazi za vijiji, kata na wilaya, pamoja na kuwajengea wanawake uwezo wa kiuchumi kupitia mafunzo ya ujasiriamali, vikundi vya uzalishaji na kutafuta masoko ya bidhaa zao.


Wakati huo huo, risala ya jukwaa hilo iliyosomwa na Katibu wa Jukwaa la Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi Wilaya ya Kishapu, Fredina Said, imebainisha mafanikio mbalimbali yaliyofikiwa tangu kuanzishwa kwa jukwaa hilo, huku ikieleza changamoto ya ukosefu wa eneo maalumu la soko kwa ajili ya wanawake wajasiriamali kuuza bidhaa zao.


Kufuatia ombi hilo, Mhe. Peter Masindi amemuagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu kutafuta eneo litakalotengwa kwa ajili ya soko la wanawake, ili kuwawezesha kufanya biashara zao katika mazingira bora ili wanawake hao waweze kufikia fursa mbalimbali za kiuchumi na kwa wepesi.


Aidha, katika kuunga mkono juhudi za jukwaa hilo, Mkuu huyo wa Wilaya ameongoza harambee iliyofanikiwa kukusanya zaidi ya Shilingi milioni 4, fedha zitakazosaidia kuimarisha mfuko wa Jukwaa la Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi Wilaya ya Kishapu.
Mbunge wa Jimbo la Kishapu Mhe. Lucy Mayenga akizungumza kwenye uzunduzi wa Jukwaa la kuwawezesha wanawake kujikwamua kiuchumi wilayani humo Julai 16, 2026 katika ukumbi wa Kishapu huku Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe. Peter Masindi akiwa ndiye mgeni rasmi
Mbunge wa Viti Maalum Vyuo Vikuu ambaye pia Mwenyekiti wa Jukwaa la Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi Mkoa wa Shinyanga, Dkt. Regina Malima akizungumza kwenye uzunduzi wa Jukwaa la kuwawezesha wanawake kujikwamua kiuchumi wilayani wilayani Kishapu Mkoani humo Julai 16, 2026 katika ukumbi wa Kishapu huku Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe. Peter Masindi akiwa ndiye mgeni rasmi
Afisa maendeleo ya jamii Mkoa wa Shinyanga Rehema Edson akizungumza kwenye uzunduzi wa Jukwaa la kuwawezesha wanawake kujikwamua kiuchumi wilayani humo Julai 16, 2026 katika ukumbi wa Kishapu huku Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe. Peter Masindi akiwa ndiye mgeni rasmi
Mwakilishi wa Mkuu wa divisheni ya Maendeleo ya Jamii Halamashauri ya Kishapu, Juma Ndoela, akisoma taarifa ya Wilaya ya Jukwaa la kuwawezesha wanawake kiuchumi kwenye uzinduzi wa jukwaa hilo wilayani humo Julai 16, 2026 katika ukumbi wa Kishapu huku Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe. Peter Masindi akiwa ndiye mgeni rasmi
Afisa Tawala wilayani Kishapu mkoani Shinyanga Fadhili Mvanga akizungumza kwenye uzunduzi wa Jukwaa la kuwawezesha wanawake kujikwamua kiuchumi wilayani humo Julai 16, 2026 katika ukumbi wa Kishapu huku Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe. Peter Masindi akiwa ndiye mgeni rasmi

Mwenyekiti wa Jukwaa la kuwawezesha wanawake kujikwamua kiuchumi wilayani Kishapu mkoani Shinyanga Pendo Sabanja akiwa kwenye uzinduzi wa jukwaa hilo wilayani humo Julai 16, 2026 katika ukumbi wa Kishapu huku Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe. Peter Masindi akiwa ndiye mgeni rasmi
Katibu wa Jukwaa la kuwawezesha wanawake kujikwamua kiuchumi wilayani Kishapu mkoani Shinyanga Fredina Said akisoma risala ya jukwaa hilo Julai 16, 2026 katika ukumbi wa Kishapu huku Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe. Peter Masindi akiwa ndiye mgeni rasmi








































































































Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com