Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Kagera, Faris Buruhani, amewataka vijana kuendelea kulinda amani na utulivu wa nchi kwa wivu mkubwa akisisitiza kuwa amani ndiyo msingi wa maendeleo ya mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla.
Faris amesema hayo alipokuwa akizungumza na vijana wa Bukoba Mjini katika mwendelezo wa Operesheni ya Vijana Daka Fursa na Samia (VIDAFUSA) inayotekelezwa na Kamati ya Utekelezaji ya UVCCM Mkoa wa Kagera.
Amesema bila amani na utulivu, juhudi za maendeleo, uwekezaji na fursa za kiuchumi kwa vijana haziwezi kufanikiwa, hivyo kila kijana ana jukumu la kuwa balozi wa mshikamano na umoja katika jamii.
Aidha, amewahimiza vijana kutumia fursa mbalimbali zinazotolewa na Serikali kujikwamua kiuchumi na kuchangia maendeleo ya Taifa badala ya kujihusisha na vitendo vinavyoweza kuhatarisha amani ya nchi.

Social Plugin