Na Mwandishi wetu Dodoma
Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) imewataka Wawekezaji kushirikiana kwenye miradi mbalimbali ambapo itaenda kuendeleza uchumi wa nchi.
Akizungumza Mkoani Dodoma kwenye Maonyesho ya wiki ya utumishi wa umma afisa uhusiano wa wakala wa majengo Tanzania (TBA) Renatus sona amesema tunawakaribisha wawekezaji wote kutoka serijalini na sekta binafsi kuja kuwekeza kwenye miradi mbalimbali.
Kupitia Maadhimisho haya tuna Wataalamu mbalimbali wa ujenzi ambao wanatoa elimu kuhusu masuala ya ujenzi wa majengo na taarifa zinahohusu zote za ujenzi.
"Tuna miradi mbalimbali mikubwa ya nyumba mkoani dodoma iliyopo Maeneo ya Nzuguni B ambapo tumejenga nyumba 3500 za watumishi wa umma."Amesema Afisa sona"
Hata hivyo tuna nyumba 150 ambazo zimekamilika kwa ajili ya watumishi wa umma ambapo tunategemea kuzindua miradi mingine hivi karibuni.
Aidha nitoe wito Kwa Wananchi Wote na wadau wanaofika kuja kutembelea Maadhimisho haya wafike kwenye banda letu kupata elimu ya Majengo.

Social Plugin