*****
Mke wa Rais wa Zanzibar, Mariam Mwinyi, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika mashindano ya Qur’an Tukufu kwa wanawake wa rika mbalimbali yatakayofanyika Jumapili katika ukumbi wa DYCCC Hall.
Mashindano hayo yameandaliwa na Umul-Muuminina Aisha Foundation (UMAIF) kwa lengo la kuhamasisha wanawake kujifunza, kusoma na kuhifadhi Qur’an Tukufu pamoja na kukuza maadili mema ya Kiislamu katika jamii.
Akizungumza kuhusu tukio hilo, Sheikh WA mkoa wa Dar es salaam, Walid Alhad Omari amewaomba Watanzania kujitokeza kwa wingi Juni 21, 2026 kushuhudia mashindano hayo yatakayowakutanisha washiriki kutoka maeneo mbalimbali.
Amesema mashindano hayo yanatarajiwa kuvutia wadau wa dini, elimu na maendeleo ya jamii, huku yakiwa jukwaa muhimu la kuhamasisha wanawake kushiriki katika kujifunza na kuhifadhi Qur’an Tukufu.









Social Plugin