Na mwandishi wetu
Serikali ya Tanzania haijauza dhahabu yoyote inayotunzwa katika Benki Kuu ya Tanzania BOT. Kauli hii imetolewa leo bungeni na Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba, wakati akijibu maswali. Hatua hii inalenga kumaliza uvumi uliokuwa unasambaa miongoni mwa wananchi kuhusu usalama wa mali hiyo ya taifa.
Ufafanuzi huo ulitokana na swali la Mbunge wa Tarime Mjini, [Esther Matiko. Mbunge huyo alitaka kujua kama kuna sehemu ya dhahabu hiyo imeshauzwa kutokana na maneno yanayovuma mitaani. Waziri Mkuu alijibu kwa msisitizo kuwa uvumi huo si wa kweli na akiba yote ipo mahali salama.
"Nitumie Bunge hili kuwahakikishia wabunge kwanza dhahabu haijauzwa mpaka sasa. Kuna wakati mawazo ya kuuza yalikuja ambapo soko lilikuwa vizuri lakini kabla ya kuuzwa bei ikashuka, Benki Kuu ikaona itakuwa hasara kuuza. Kwahiyo hawakuuza kwasababu bei ilishuka. Lakini mantiki yake ni nini? Ni kama ambavyo inafanya kwenye dola, kwamba kuna wakati Benki Kuu inauza dola kama sehemu ya kuyapatia maben

Social Plugin