Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

RAIS SAMIA AUNDA TUME YA UCHUNGUZI WA KIJINAI VURUGU UCHAGUZI MKUU 2025 KUONGOZWA NA JAJI SHABANI LILA

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameunda Tume ya Uchunguzi wa Kijinai wa Matukio ya Ghasia ya Wakati na Baada ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025. 

Hatua hiyo imechukuliwa katika kutekeleza mapendekezo ya Tume ya Rais ya Kuchunguza Matukio ya Uvunjifu wa Amani yaliyotokea katika kipindi hicho cha uchaguzi.  

Katika taarifa rasmi iliyotolewa leo tarehe 18 Mei, 2026 na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Dkt. Moses M. Kusiluka, Rais ameteua viongozi na wajumbe wa tume hiyo kwa kuzingatia mamlaka aliyonayo chini ya Sheria ya Tume za Uchunguzi, Sura ya 32.  

Katika uteuzi huo, Jaji wa Mahakama ya Rufani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Shabani Ally Lila, ameteuliwa kuwa Kamishna na Mwenyekiti wa Tume hiyo. 

Uzoefu wake katika mambo ya kisheria unatajwa kuwa nguzo muhimu katika kuongoza uchunguzi huo wa kijinai. 

 Aidha, Rais Samia ameteua majaji wastaafu watatu wa Mahakama Kuu ya Tanzania kuwa Makamishna wa tume hiyo ili kushirikiana na Mwenyekiti. Makamishna walioteuliwa ni Mhe. Gad John Mjemmas, Mhe. Awadh Mohamed Bawazir, pamoja na Mhe. Aishieli Nelson Sumari. Tume hii inatarajiwa kuanza kazi mara moja ili kuleta majibu na mapendekezo ya kisheria kuhusu ghasia hizo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com