Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

WALIOSEMA 'WAMEGUSWA BEGA NYETI ZAO ZIKAPOTEA KIMIUJIZA' WATUPWA JELA SHINYANGA

Watu wawili wakazi wa Manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga wamehukumiwa kifungo cha jela baada ya kupatikana na hatia ya kusambaza taarifa za uongo zilizosababisha taharuki katika jamii.

Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari leo Aprili 9, 2026, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, SACP Janeth Magomi, aliwataja waliohukumiwa kuwa ni Kisaka Elininhaki (22), mfanyabiashara, pamoja na Makoye James (20), dereva.

Kwa mujibu wa Kamanda Magomi, watuhumiwa hao walikamatwa baada ya kusambaza taarifa zisizo za kweli wakidai kuwepo kwa siri iliyopotea kimujiza baada ya kuguswa na benga, hali iliyozua hofu na taharuki kwa wananchi.

Ameeleza kuwa baada ya kufikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Kahama, wawili hao walipatikana na hatia ya kusambaza taarifa za uongo.

Katika hukumu iliyotolewa, Kisaka Elininhaki amehukumiwa kifungo cha miezi sita jela, huku Makoye James akihukumiwa kifungo cha miezi mitano jela.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga limewakumbusha wananchi kuwa kusambaza taarifa za uongo ni kosa la jinai na linaweza kusababisha madhara makubwa kwa jamii. 

Aidha, wananchi wametakiwa kutoa taarifa sahihi na kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama ili kudumisha amani na utulivu.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com