
"Nimepokea kwa masikitiko taarifa ya kifo cha Mbunge wa Jimbo la Peramiho, Mheshimiwa Jenista Joakim Mhagama. Ninatoa pole kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Mussa Azzan Zungu, wananchi wa Jimbo la Peramiho, familia, ndugu, jamaa na marafiki.
Kwa miaka 38, Mheshimiwa Mhagama amekuwa mwanachama mahiri wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), kiongozi wa vijana, kiongozi wa wanawake, waziri katika awamu mbalimbali na mnasihi wa wengi katika siasa na maisha.
Mwenyezi Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi.
Amina"_ Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Social Plugin