
Padre wa Parokia ya Mt. Yohane Maria Vianney -Mhunze,Jimbo Katoliki la Shinyanga Baba Paroko. Josephat Mahalu akizungumza kwenye misa ya shukrani ya jumuiya ya Mt.Yuda Thadei Parokia ya Mtakatifu Yohane Maria Vianney- Mhunze Wilayani Kishapu mkoani Shinyanga Novemba 22,2025
Na Sumai Salum – Kishapu
Jumuiya ya Mt. Yuda Thadei Parokia ya Mhunze, kanisa la Mtakatifu Yohane Maria Vianney- Mhunze Wilayani Kishapu mkoani Shinyanga, imefanya misa maalumu ya kumshukuru Mungu kwa kuendelea kulitunza Taifa la Tanzania na kuilinda jamii dhidi ya maovu mbalimbali.
Akizungumza katika ibada hiyo, Novemba 22,2025 Padre wa Parokia ya Mt. Yohane Maria Vianney Baba Paroko, Josephat Mahalu amesema umuhimu wa misa hiyo ni kurudisha utukufu kwa Mungu kwa yote makubwa anayoyatenda kwa Taifa na kwa familia. Amesema ibaada za shukrani ni chanzo cha baraka zaidi kwa sababu Mungu hujibu pale anapotambua moyo wa shukrani kutoka kwa watu wake.
“Kanuni ya shukrani inamfanya anayeshukuriwa atende zaidi, kwani anaona thamani yake imetambuliwa,” amesema Padre Mahalangu.
Misa hiyo iliyofanyika nyumbani kwa Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Mhe. Peter Masindi, ambaye amepata nafasi ya kumshukuru Mungu kwa kuendelea kumlinda na kuwalinda wananchi wa kishapu kwa kuendelea na shughuli zao za uzalishaji mali kwa amani na utulivu.
Baadhi ya waumini na washiriki wa misa hiyo wamepongeza hatua hiyo, wakisema ni mfano mzuri unaopaswa kuigwa na jamii nzima, kwa kuwa Mungu hujibu maombi ya wenye haki na wanaomkiri kwa moyo wa unyenyekevu.
Sambamba na hayo, misa hiyo takatifu imehudhuriwa pia na Padre wa parokia ya Ndoleleji, Baba Paroko Emmanuel Ndoma na Padre wa Parokia ya Wila, Baba Paroko Paschal Mahalagu, wanajumuiya wa jumuiya ya Mt.Yuda Thadei,baadhi ya wanachi wa Kishapu, watumishi mbalimbali, viongozi wa kisiasa wilayani humo, viongozi wa dini mbali pamoja na watoto wanaoishi katika mazingira magumu ndani ya Wilaya ya Kishapu.

Padre wa Parokia ya Wila, Jimbo Katoliki la Shinyanga,Baba Paroko Paschal Mahalagu akihubiri kwenye misa ya shukrani ya jumuiya ya Mt.Yuda Thadei Parokia ya Mtakatifu Yohane Maria Vianney- Mhunze Wilayani Kishapu mkoani Shinyanga Novemba 22,2025

Padre wa parokia ya Ndoleleji Jimbo Katoliki la Shinyanga, Baba Paroko Emmanuel akizungumza kwenye misa ya shukrani ya jumuiya ya Mt.Yuda Thadei Parokia ya Mtakatifu Yohane Maria Vianney- Mhunze Wilayani Kishapu mkoani Shinyanga Novemba 22,2025

Mkuu wa Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga na mwanajumuiya ya Mt.Yuda Thadei Parokia ya Mt. Yohane Maria Vianney -Mhunze Mhe.Peter N. Masindi akizungumza kwenye misa hiyo































Social Plugin