
Mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga SC, wameendelea kutamba baada ya kuibuka na ushindi mwembamba wa bao 1–0 dhidi ya AS FAR Rabat katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika uliopigwa leo, Novemba 22, 2025, kwenye Dimba la New Amaan Complex, Zanzibar.
Bao hilo pekee lililowapa furaha Wananchi lilifungwa na mshambuliaji Prince Dube dakika ya 58, akimalizia kwa ustadi pasi murua ya kiungo Mudathir Yahya, ambaye alionesha ubunifu wa hali ya juu katikati ya uwanja.
Kwa matokeo hayo, Yanga SC imejikusanyia pointi tatu muhimu katika uwanja wao wa nyumbani, hatua inayowapa nafasi nzuri ya kujiongezea matumaini ya kusonga mbele kwenye hatua za juu za michuano hiyo mikubwa barani Afrika.
Social Plugin