Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MAWAZIRI WALIOWEKWA PEMBENI BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ametangaza baraza jipya la mawaziri ambalo limeleta mchanganyiko wa sura mpya na mabadiliko makubwa katika nafasi mbalimbali za uongozi wa serikali.

Katika mabadiliko hayo, baadhi ya mawaziri na manaibu waliohudumu kwenye baraza lililopita hawajarejeshwa, hatua inayoashiria mwelekeo mpya wa utendaji na maboresho katika mfumo wa Serikali.

Miongoni mwa viongozi walioachwa nje ya baraza jipya ni aliyekuwa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko, pamoja na mawaziri kadhaa akiwamo Hussein Bashe (Kilimo), Innocent Bashungwa (Mambo ya Ndani), Jenista Mhagama (Afya), Dkt. Seleman Jafo (Viwanda na Biashara), Dkt. Pindi Chana (Maliasili na Utalii) na Dkt. Damas Ndumbaro aliyekuwa Waziri wa Katiba na Sheria.

Baraza hili jipya linatarajiwa kuleta kasi mpya katika utekelezaji wa sera, usimamizi wa rasilimali, na kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi, sambamba na kusimamia vipaumbele vya serikali katika kipindi kijacho.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ametangaza Baraza la Mawaziri





Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com