
Meneja wa NMB tawi la Chalinze, Mbaruku Nyenga

Mkurugenzi wa Albertho day care & Albertho stationery Bw. Albertho Mbugano
*****
NA. ELISANTE KINDULU, CHALINZE
TAASISI ya NMB tawi la Chalinze na Albertho stationery & Albertho day care centre wamechaangia vifaa mbalimbali katika shule ya msingi Bwilingu A, mjini Chalinze.
Vifaa hivyo vimetolewa jana katika mahafali ya 44 ya darasa la saba yaliyofanyika katika viwanja vya shule hiyo na kuhudhuriwa na mamia ya wananchi walioshereheshwa na vikundi mbalimbali vya sanaa.
Mgeni rasmi Bw. Albertho Mbugano ambaye anamiliki vituo vya kulelea watoto (Albertho day care) pamoja na kuuza na kutoa huduma za kiofisi (stationery) aliwaambia wazazi shuleni hapo kushiriki kikamilifu kuchangia maendeleo shuleni ili kuunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya sita katika kuleta maendelo ya elimu nchini.
Bw. Albetho alitoa kompyuta 1 na mipira 5 huku meneja wa NMB tawi la Chalinze akichangia mipira 2 na vifaa vya kihisabati kwa wanafunzi wa darasa la saba waliofanya vizuri kitaaluma, licha ya wazazi kujitokeza katika harambee ya kuchangia fedha kwaajili ya ununuaji wa viti kwaajili ya walimu ofisini.
Akisoma risala muda mfupi kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi, mwalimu mkuu wa shule hiyo Wilfred Mugisha alieleza kuwa shule imekuwa na mafanikio mbalimbali ikiwemo kuongezeka kwa ufaulu wa matokeo ya darasa la saba kila mwaka.
"Licha ya mafanikio hayo lakini shule yetu inakabiliwa na upungufu wa samani za ofisini, vifaa vya michezo na uhitaji wa kompyuta na mashine ya kurudufu", alisema.










Social Plugin