
MGOMBEA ubunge wa Jimbo la Hanan'g Asia Halamga wa Chama cha Mapinduzi(CCM) amemuomba mgombea urais wa CCM Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwajengea kiwanda cha nafaka wilaya ya Hanan'g ili vijana waweze kupata ajira.
Asia ametoa ombi hilo leo Oktoba 3 wakati akiomba ridhaa ya kuchaguliwa kuwa mbunge katika uwanja wa Mlima Hanan'g uliopo Katesh.
"Hapa tuna mazao ya kilimo na chumvi tunaomba utujengee viwanda watu wapate ajira,"amesema Asia
Aidha amesema wilaya hiyo haina shida ya huduma za kijamii wanaomba wajengewe kiwanda cha nafaka ili watu wapate ajira na kukuza uchumi wao.
Ametumia fursa hiyo kumhakikishia mgombea wa urais kuwa wananchi wa hapo watampatia kura za kutosha.
Naye mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi(CCM) mkoa wa Manyara Peter Toima amemhakikishia mgombea wa urais kuwa watampatia kura kwa asilimia 100 huku Waziri Mkuu Mstaafu Fredrick Sumaye akimpa uhakika kuwa wananchi watampa kura kwa zaidi ya asilimia 90.
Social Plugin