
Na Jaliwason Jasson, HANAN'G
MGOMBEA urais wa Chama cha Mapinduzi(CCM) Dkt. Samia Suluhu Hassan ameahidi kuwajengea barabara wananchi wa wilaya ya Hanan'g ili kurahisisha usafirishaji wa mazao.
Dk. Samia amesema atajenga barabara ya Nangwa/Gisamgalang kuelekea Kondoa kilometa 79 na barabara nyingine ni ya Mogitu/Haydom kilometa zaidi ya kilometa 80.
Amesema barabara hizo zitapitika muda wote iwe jua au iwe mvua.
Wakati huo huo ameahidi wafugaji kupata soko la wanyama hai.
"Tumepata soko la nyama tulikuwa tunakosa soko kwa kuwa tulikuwa hatuchanji mifugo yetu sasa tunachanja.
Amewaambia wananchi nyama itapata soko lipo kutoka nje ya Nchi.
Mgombea huyo amesema ataendelea kutoa ruzuku kwa wafugaji ili mifugo inayozalishwa iwe na tija.
Social Plugin