
Mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha ACT Wazalendo, Mhe. Luhaga Mpina, amewataka watia nia wa nafasi za udiwani na ubunge kupitia chama hicho kuhakikisha wanasimamia kwa ukamilifu kura zitakazopigwa kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu, ili kukiwezesha chama hicho kushinda kwa kishindo.
Akizungumza leo Agosti 18, 2025 katika zoezi la kuomba udhamini wa kuwania nafasi ya urais mkoani Shinyanga, Mpina amesema ni muda wa kuhakikisha ACT Wazalendo inapata viongozi wengi bungeni, kwenye udiwani, na kushinda urais kwa kuwa na mawakala makini watakaolinda kura.
“Tunakwenda kutangaza kiama cha mateso waliopata watanzania, kwa kazi moja tu ya kuwaunga mkono makada wa ACT Wazalendo ili waweze kutatua matatizo sugu, yaliyogeuzwa kuwa bidhaa ya kuwaingizia watu kipato, tutakwenda kuifanya hiyo kazi kwa muda wa siku 60”, amesema Mpina.
“Tutapita kwenye majimbo yote bara na visiwani kwaajili ya kuziomba kura za watanzania kuwaambi ukweli tunataka tuioneshe dunia kuwa inawezekana kufanya mabadiliko kwa muda mfupi”, ameongeza Mpina.
Ameongeza kuwa chama hicho kitapita kwenye majimbo yote bara na visiwani kwa ajili ya kuomba kura na kuwaeleza Watanzania ukweli, huku akisisitiza kuwa lengo ni kuonesha dunia kwamba mabadiliko yanawezekana kwa muda mfupi.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Ngome ya ACT Wazalendo, Abdul Nondo, amesema kwa mujibu wa Katiba Ibara ya 61, wananchi wanaruhusiwa kuchagua wabunge wa kuisimamia serikali, hivyo uchaguzi wa mwaka huu utakuwa wa kihistoria kwa kuonesha mamlaka ya wananchi.
Naye mtia nia wa ubunge jimbo la Shinyanga Mjini, Ndugu Emmanuel Ntobi, ameeleza changamoto zinazowakabili wananchi wananchi wa mkoa wa Shinyanga, hususan wakulima wa zao la pamba na vyama vya ushirika, huku wanachama wa chama hicho wakibainisha dhamira yao kubwa ya kumdhamini Mhe. Luhaga Mpina kuwania nafasi ya urais wa Tanzania.
Mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha ACT Wazalendo, Mhe. Luhaga Mpina akizungumza na wanancham wa chama hicho Shinyanga Mjini.
Mtia nia wa Ubunge jimbo la Shinyanga Mjini, Ndugu Emmanuel Ntobi kipitia chama hicho akizungumza.
Mwenyekiti wa Ngome ya ACT Wazalendo, Abdul Nondo akizungumza.











Social Plugin