Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

DOTTO BAHEMU MGOMBEA PEKEE NAFASI YA UBUNGE JIMBO LA NGARA BAADA YA CHAUMA KUSHINDWA KUREJESHA FOMU*

Dotto Bahemu mgombea Ubunge Jimbo la Ngara

Na Mariam Kagenda _ Kagera  

Mgombea Ubunge Jimbo la Ngara kupitia Chama Cha Mapinduzi   Dotto Bahemu ni Mgombea pekee katika  Jimbo hilo baada ya Chama Cha Ukombozi wa Umma kushindwa kurejesha fomu na vyama vingine kutochukua fomu ya kugombea katika nafasi hiyo 

Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Ngara Bwana Constantino Msemwa wakati akizungumza na Mwandishi amesema kuwa waliochukua fomu ya kugombea nafasi ya Ubunge katika Jimbo hilo ni wawili ambao ni Dotto Jasson  Bahemu kutoka Chama Cha Mapinduzi na Peter Ruzige kutoka Chama Cha Ukombozi wa Umma lakini mpaka wakati wa kufungwa kwa zoezi la uchukuaji na urejeshaji wa fomu aliyerudisha  ni Jasson Bahemu pekee.

Amesema kuwa Dotto Bahemu ametimiza vigezo  vyote vinavyotakiwa  Kikatiba ,Kisheria ,Kikanuni na kuwasilisha  nyaraka sahihi   hivyo Tume huru ya Taifa  ya Uchaguzi  imemteua kuwa Mgombea wa nafasi ya Ubunge Jimbo la Ngara .

Ameongeza kuwa Vyama vingine havikujitokeza kuchukua fomu ya kugombea nafasi ya Ubunge katika Jimbo la Ngara isipokuwa Chama cha Mapinduzi(CCM) pamoja na Chama Cha Ukombozi wa Umma ( CHAUMMA) pekee ndiyo vilivyojitokeza katika zoezi hilo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com