Naibu Katibu Mkuu wa Habari, Mawasiliano na TEHAMA Dkt. Jim Yonazi akiongea wakati wa ufunguzi wa warsha ya watoa huduma za Posta nchini ikiwa ni wiki ya Posta Duniani.
Naibu Katibu Mkuu wa Habari, Mawasiliano na TEHAMA Dkt. Jim Yonazi akiongea wakati wa ufunguzi wa warsha ya watoa huduma za Posta nchini ikiwa ni wiki ya Posta Duniani.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Dkt. Jabir Bakari akiongea kwenye warsha hiyo ambao ameeleza TCRA ilivyojidhatiti kuongeza wigo huduma za Posta kwa Jamii.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Dkt. Jabir Bakari akiongea kwenye warsha hiyo ambao ameeleza TCRA ilivyojidhatiti kuongeza wigo huduma za Posta Kwa Jamii.
Baadhi ya washiriki wa warsha ya watoa huduma za posta nchini wakisikiliza kwa makini masuala mbalimbali yanayohusu huduma za Posta.
***
Na Dotto Kwilasa, Dodoma
TANZANIA ikiwa inaadhimisha wiki ya Posta Duniani, Serikali imesema inaendelea kuongeza ubunifu katika kuboresha huduma za Posta nchini kuendana na ulimwengu wa Sayansi na Teknolojia ikiwa ni pamoja na kuhakikisha nchi nzima inafikiwa na mfumo wa anuani za makazi kurahisisha utambuzi na utoaji huduma bora kwa jamii.
Hayo yamesemwa leo Oktoba 7,2021,Jijini Dodoma na Naibu Katibu Mkuu wa Habari, Mawasiliano na TEHAMA Dkt. Jim Yonazi wakati akifungua warsha ya watoa huduma za Posta nchini ,huku akisisitiza kuwa ni muhimu kuleta ubunifu kuwezesha utoaji huduma na ufikishaji wa vifurushi na vipeto katika maeneo ya makazi, ofisi na sehemu za biashara.
Aidha amesema ubunifu huo utasaidia pia utoaji wa huduma nyingine za jamii zikiwemo huduma za kutoa taarifa kwa zima moto na polisi .
Akiongea kwenye warsha hiyo iliyoandaliwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Dkt.Yonazi amesema hadi sasa jumla ya Halmashauri ishirini na moja tayari zimefikiwa na huduma ya anuani za Makazi na kwamba kinachoendekea kwa sasa ni kuunganisha mfumo huo Kwa nchi nzima.
“Ili kuendelea kiuchumi lazima tutumie huduma za Posta nchini,kila mtu atambue umuhimu wake Katika kukuza uchumi wetu,faida kubwa ya posta inawezesha bidhaa moja kutoka sehemu moja mpaka nyingine na usafirishaji wa mizigo bado unabaki kuwa ni kitu muhimu,"amesema.
Licha ya hayo ameeleza kuwa Serikali imeeneza Postikodi katika Halmashauri 21 nchini na mipango inaendelea kuweka katika maeneo mengine hali itakayosaidia mizigo kufika kila mahali,kwa wakati na bila ubabaishaji.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Dkt. Jabir Bakari amesema warsha hiyo ni muhimu kwani hutoa huduma ya kusafirisha mizigo kwa umakini huku akisisitiza kuwa TCRA imejidhatiti kuhakikisha huduma za posta nchini inakuwa ya ushindani kwa shabaha ya kuongeza wigo wa utoaji huduma badala ya kuachia huduma hizo kwa watumiaji wachache.
"Huduma za posta zilizoboreshwa ni muhimu kwa Maendeleo ya nchi, kwa kuzingatia kuwa zinawezesha mabadilishano ya bidhaa za biashara zinazowezesha ukuaji wa uchumi wa Viwanda,lazima jamii itambue kuwa kuendesha biashara kidigitali ni nguzo kuu ya mabadiliko ya kiuchumi,"amesema.
Social Plugin