PROF. MWANDOSYA : SUGU UMEHITIMU CHUO CHA UANASIASA

TANGAZA BIASHARA,HABARI,KAZI,MATUKIO YAKO KUPITIA MALUNDE 1 BLOG,TUPIGIE SIMU 0757 478 553 AU 0625 918 527

Waziri wa serikali ya awamu ya nne Prof. Mark Mwandosya ameingia katika Orodha ya watu walioonesha furaha yao baada ya Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi kuachiliwa jana kutoka gerezani ambapo alihukumiwa kifungo cha miezi mitano.


Prof. Mwandosya ameandika katika ukurasa wake wa twitter; “Nikimpa hongera Mbunge wa Mbeya Joseph Mbilinyi kwa kuhitimu Chuo cha Uanasiasa, gereza la Ruanda, Mbeya. Kutofautiana vyama, itikadi na misimamo kusilete uhasama na uadui. Mungu Ibariki Tanzania.”
Theme images by rion819. Powered by Blogger.