SERIKALI YATANGAZA NAFASI ZA KAZI 6,180

Serikali imetangaza nafasi za kazi zaidi ya 6,180 katika sekta ya afya nchini na kuwataka wananchi wenye sifa stahiki kuomba nafasi hizo ili kuweza kutatua changamoto ya upungufu wa watumishi katika vituo vya Afya, Zahanati na Hospitali za Wilaya.

Akiongea na waandishi wa habari jana Mei 10, 2018 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Selemani Jafo alisema watumishi hao wataajiliwa kabla ya mwaka kuisha na kuongeza kwamba lengo la serikali ni kuboresha sekta ya afya nchini.

“Naomba niwataarifu kwamba serikali ofisi ya TAMISEMI imepata kibari cha kuajiri watumishi wapya 6,180, watumishi hawa tunatarajia kuwa ajiri hivi karibuni kabla ya mwaka huu kuisha kwa hiyo napenda kuutangazia umma kuwa dirisha la ajira lipo wazi, kwa watu wote wenye sifa kuhakikisha wanaomba nafasi hizo lengo kubwa ni kupata watumishi kwaajili ya vituo vya afya vipya tunavyovijenga” alisema Jafo.

Waziri Jafo amliongeza kuwa watumishi waliokua wanajitolea watapewa kipaumbele zaidi; “kuna vijana wengine wamemaliza taaluma yao na hawataki ipotee wameamua kuomba nafasi mbalimabi kwa ajili ya kujipa uzoefu kwahiyo watu hao watakua kipaumbele chetu cha kwanza katika kuwaingiza katika ajira”

Waziri wa Tamisemi amesema serikali inakamilisha ujenzi wa vituo vya afya 208 ambavyo vitagharimu shilingi bilioni 156 katika ujenzi wa miundombinu na vifaa tiba, pia serikali inajenga hospitali kubwa za wilaya takribani 68 na zitagharimu shilingi bilioni 105.

Watakaoajiriwa ni wenye sifa zifuatazo, Awe raia wa Tanzania, kuambatanisha nakala ya cheti cha kuzaliwa, kidato cha nne na sita, cheti cha taaluma na asiwe muajiliwa wa serikali au shirika la dini ambapo mshahara wake unalipwa na serikali, umri usizidi miaka 45 na utayali wa kufanyakazi mahali popote nchini

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527