Breaking : LULU ATOLEWA GEREZANI


Habari njema kwa wapenzi na mashabiki wa Muigizaji Elizabeth Michael, maarufu Lulu leo Jumatatu Mei 14,2018 ni kwamba mrembo huyo amebadilishwa kifungo na sasa atatumikia adhabu hiyo akiwa nje yaani ‘kifungo cha nje’.

Ofisa Habari wa Jeshi la Magereza, Lucas Mboje amesema Lulu amebadilishiwa adhabu na atatumikia kifungo cha nje kwa amri ya Mahakama Kuu ya Tanzania, Dar es Salaam.

“Lulu amebadilishiwa adhabu na ameachiwa juzi Jumamosi kati ya saa 2 hadi 3 asubuhi. Hii si kwamba ameachiwa huru, bali amebadilishiwa adhabu na atatumikia kifungo chake nje, kitaalamu tunaita ‘community service” ,amesema Mboje

Lulu alihukumiwa kifungo cha miaka miwili jela Novemba mwaka jana baada ya kupatikana na hatia ya kumuua bila kukusudia msanii mwenzake, Steven Kanumba.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527