EBITOKE AANZISHA VITA NA SHILOLE...AMMWAGIA POVU

TANGAZA BIASHARA,HABARI,KAZI,MATUKIO YAKO KUPITIA MALUNDE 1 BLOG,TUPIGIE SIMU 0757 478 553 AU 0625 918 527

Mchekeshaji maarufu kutoka Timamu Tv, Ebitoke ameibuka na kumtolea povu zito Shilole huku akidai kuwa hamuelewi kama ni msanii au mama ntilie maana hajui kazi yake hata moja.


Kwenye mahojiano aliyofanya na kipindi cha Kikaangoni cha East Africa Tv, Shabiki mmoja alimtaka ataje wimbo mmoja wa Shilole na kuuimba ndipo aliposema hajui wimbo wake hata mmoja kwani hajui kama ni msanii au ni mama ntiliye:


"Labda unitajie nyimbo zake mimi sijui kazi zake mimi najuaga yeye ni mpishi tu ila hapa Kwenye nyimbo mtanisamehe kwa kweli sizijui nyimbo zake…..Nisiwe muongo naongea ukweli wala sio kiki kama mlivyozoea mambo ya kiki siku hizi nimeacha”.


Shilole mbali ya kuwa msanii wa Bongo fleva Lakini pia ni mfanyabiashara ambaye anamiliki mgahawa wake unaoitwa Shishi Food ambapo anauza vyakula mbali mbali.
Theme images by rion819. Powered by Blogger.