MAELFU WAJITOKEZA KUMZIKA MASOGANGE HUKO MBEYA ,TAZAMA PICHA & VIDEO HAPA





Safari ya mwisho duniani ya aliyekuwa msaani maarufu aliyekuwa akipamba video za wanamuziki wa Bongo fleva, Agnes Gerald 'Masogange' imehitimishwa jana saa tisa alasiri bada ya kuhifadhiwa kwenye nyumba ya milele nyumbani kwa wazazi wake Utengule – Mbalizi mkoani Mbeya.


Maelfu ya waombolezaji kutoka Dar es salaam na maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Mbeya walijitokeza wakiongozwa na Mkuu wa mkoa huo, Amos Makalla.


Akitoa salamu za rambirambi kutoka serikalini, Makalla amesema hakuna mtu anayejiandaa wala aliye tayari kwa ajili ya kifo, hivyo kifo cha Masongange ni kilelezo kwamba binadamu wote hapa duniani ni wasafiri.


‘Kifo cha Masogange kitukumbushe kwamba sote tutakufa, nimefurahi namna wasanii mlivyojipanga bila kujali bifu na tofauti zenu, katika hili mmekuwa pamoja,” amesema Makalla.


“Nilikuwa nafuatilia tangu msiba huu ulipotokea, mlikuwa pamoja na kwa mshikamano na sisi Serikali tunawapa pongezi sana.”


Makalla amewapongeza wananchi kwa namna walivyojitokeza kwa wingi na hiyo inaonyesha ndio utamaduni wa Mtanzania kushirikiana katika matatizo.


Akimshukuru Makalla kwa niaba ya wasanii wenzake, mwenyekiti wa wasanii hao, Steve Nyerere amesema, “hili ni pigo kwetu wasanii. Na sisi kama wasanii tumekubaliana kiasi tulichojichanga, kiasi fulani kitatumika kumlipia ada ya mwaka mmoja mtoto wa marehemu ambaye yupo darasa la saba lakini pia kumlipia bima ya afya endelevu.”

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527