DR. CHENI AFUNGUKA MAZITO KUHUSU MAISHA YA LULU GEREZANI

Muigizaji mkongwe wa Bongo movie Dr. Cheni amefunguka mazito juu ya maisha ya Elizabeth Michael ‘Lulu’ gerezani.

Ni miezi kadhaa tangu Lulu aende jela baada ya kuhukumiwa miaka miwili baada ya kupatikana na hatia ya kumuua bila kukusudia aliyekuwa mpenzi wake marehemu Steven Kanumba.

Wiki iliyopita tuliona jinsi Dr. Cheni alivyomuwakilisha Lulu kwa kutoa msaada kwenye kampenzi ya Namthamini ya EATV. Dr. Cheni ni mtu ambaye siku zote amekuwa na ukaribu sana na Lulu hadi Lulu humuita Baba yake.

Kwa mara nyingine Tena Dr. Cheni amefunguka kuhusu maisha ya Lulu gerezani ambapo kwenye mahojiano na Millard Ayo Tv amefunguka haya:

"Kusema ukweli Lulu ni binti jasiri sana yaani sisi tuliokuwa nje tuna majonzi kuliko yeye mwenyewe 

"Yaani ukienda unamkuta ana furaha mtacheka naye mtafurahi, kikubwa anasema tu niombeeni basi na kitu kikubwa Lulu huko jela anatizama sana mabinti, anasema anawapenda sana mabinti wa Kitanzania”.

Lakini pia Dr. Cheni amesema kuwa Lulu ana kawaida sana ya kutoa misaada ingawa hapendi kujitangaza Kwenye mitandao ya kijamii pia amedai Miezi michache kabla hajahukumiwa alienda kutoa msaada segerea.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527