WAZIRI ATUMBULIWA KWA KUMCHAPA KIBAO MBUNGE

Bunge la Zambia limemsimamisha waziri kwa muda wa mwezi mmoja asihudhurie vikao kutokana na kosa la kumpiga mbunge kwenye viwanja vya Bunge.

Spika wa Bunge la Taifa, Patrick Matibini amesema Waziri wa Jimbo la Lusaka, Bowman Lusambo amesimamishwa baada ya kumchapa kibao mbunge Chishimba Kambwili hapo Oktoba mwaka jana, na kusema kwamba tabia hiyo haikubaliki dhidi ya mbunge.

"Hili ni Bunge la heshima, nina wajibu wa kuhakikisha kwamba heshima na haiba ya Bunge inalindwa na inahifadhiwa wakati wote," amesema spika huyo.

Kutokana na kusimamishwa huko Waziri Lusambo hatapata marupurupu na mshahara kama mbunge kwa mwezi wote anaotumikia adhabu.

Imeelezwa kwamba ni jambo la kawaida kwa wabunge kutumia lugha isiyofaa na kuleta mizozo, lakini kwa kitendo cha Waziri kumpiga mbunge hakikuwa cha kuvumilika.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527