VIONGOZI WA MTANDAO WA WANAFUNZI TANZANIA WAHOJIWA NA DCI SAKATA LA NONDO

Mpaka kufikia leo Machi 14, 2018 saa 7:45 mchana viongozi wawili wa Mtandao wa Wanafunzi Tanzania (TSNP) walikuwa wamekwisha hojiwa na Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI).


Ofisa habari wa mtandao huo Helleh Sisya ambaye naye pia miongoni mwa watakaohojiwa, amesema hadi muda huo waliohojiwa ni mkaguzi wa haki za binadamu , Alphonce Lusako na katibu wa mtandao huo, Malekela Brigthon.


Viongozi wengine ambao hawajahojiwa hadi muda huu ni Sisya na mkurugenzi wa Idara ya sheria, Paul Kisabo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527