Mambo ni Motooo!! FILAMU YA "LAANA YA MKE" KUZINDULIWA KESHO IJUMAA MACHI 23


Mwaka mmoja baada ya kuachia Filamu ya ‘Nyama ya Ulimi’,Bongo Movies Shinyanga wanakuletea Filamu nyingine kali inaitwa “Laana ya Mke” ambayo itazinduliwa rasmi kesho Machi 23,2018.


Tayari wageni mbalimbali wakiwemo wasanii maarufu wa filamu nchini,viongozi wa bodi ya filamu wameshaanza kuwasili mjini Shinyanga kwa ajili ya kushuhudia uzinduzi wa filamu hii ambayo imekuwa gumzo kila kona.

Mwenyekiti wa Bongo Movies Shinyanga Juma Ibrahim Songoro ameiambia Malunde1 blog kuwa uzinduzi wa filamu ya Laana ya Mke utafanyika kesho tarehe  23.03.2018 katika ukumbi wa NSSF ya zamani “CCM mkoa wa Shinyanga” kuanzia saa tatu usiku.


Katika Filamu hii iliyoongozwa na Director mahiri Dave Skerah wamo Magwiji wa Filamu akiwemo Blandina Chagula ‘Johari’, Ibrahim Songoro ‘Songoro Gadafi’,Magreth Emmanuel, Mariam Bilal, Najma Shahel,Edward Joseph na Mzee Salum Kawelewele.


Filamu hiyo yenye ubora wa hali ya juu inahusu majanga na laana wanazopata wanaume wababe,wasio na fadhila wanaotafuta mali na wake zao kisha kuwafanyia ukatili.

TUMIA DAKIKA ZAKO 2 TU KUANGALIA KIONJO CHA FILAMU YA LAANA YA MKE



Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527