RAIS MAGUFULI AWAAPISHA DR SLAA NA MBOWETO KUWA MABALOZI WA SWEDEN, NIGERIA


Leo Februari 16, 2018 Rais John Magufuli amewaapisha mabalozi wawili aliowateua kuiwakilisha Tanzania katika nchi za Nigeria na Sweden.

Taarifa iliyotolewa leo na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi inaeleza kuwa walioapishwa ni Muhidin Ally Mboweto ambaye ameteuliwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Nigeria na Dk Willbrod Peter Slaa ambaye ameteuliwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Sweden.

Uteuzi wa Mabalozi hao kuiwakilisha Tanzania katika nchi walizopangiwa umeanza jana Februaru 15, 2018.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527