RAIS MAGUFULI APAKWA MAJIVU IBADA YA JUMATANO YA MAJIVU

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipakwa majivu wakati wa ibada ya Jumatano ya Majivu katika kanisa la Mtakatifu Joseph jijini Dar es salaam asubuhi ya leo.

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ameungana na waumini wa Kanisa Katoliki na wakristo wengine katika ibada ya Jumatano ya majivu inaoashiria kuanza kwa mfungo mtukufu wa kwaresma.

Magufuli akiwa na mkewe, Mama Janeth Magufuli wameungana na waumini hao katika ibada iliyoongozwa na Muadhama Askofu Mkuu, Polycarp Kardinali Pengo wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam katika Kanisa la Mtakatifu Joseph, Dar es salaam, leo Februari 14, 2018.
Rais John Magufuli akisalimiana na Muadhama Askofu Mkuu Polycarp Kardinali Pengo wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam baada ya kujiunga na waumini wengine katika ibada ya Jumatano ya Majivu katika kanisa la Mtakatifu Joseph jijini Dar es salaam asubuhi ya leo Feb 14.
Mama Janeth Magufuli akisalimiana na Muadhama Askofu Mkuu Polycarp Kardinali Pengo wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam baada ya kujiunga na waumini wengine katika ibada ya Jumatano ya Majivu katika kanisa la Mtakatifu Joseph jijini Dar es salaam asubuhi ya leo Feb 14,2018.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527