RAIS MAGUFULI AMLILIA MZEE KINGUNGE ...ASEMA ALIKUWA NA MCHANGO MKUBWA SANA KWENYE TAIFA


Rais John Pombe Magufuli amepokea kwa huzuni na masikitiko taarifa za kifo cha mwanasiasa mkongwe nchini Tanzania Mzee Kingunge Ngombale Mwiru kilichotokea leo alfajiri Ijumaa Februari 2,2018 wakati akipatiwa matibabu katika hospitali ya taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam.

Mzee Kingunge alikuwa akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili baada ya kushambuliwa na mbwa nyumbani kwake Jijini Dar es Salaam takriban mwezi mmoja uliopita.

Katika salamu zake rais Magufuli amesema taifa limepoteza mtu muhimu ambaye alitoa mchango mkubwa katika kupigania uhuru na baada ya kupata uhuru akiwa mtumishi mtiifu wa chama cha TANU na baadaye CCM na katika nyadhifa mbalimbali za serikali.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527