MTULIA: MKINIKOPESHA KURA ZENU, NITAWALIPA MAENDELEO


Mgombea Ubunge jimbo la Kinondoni kwa tiketi ya CCM, Ndugu Maulid Said Mtulia akinadi sera zake jukwaani eneo la Msufini kata ya Mwananyamala.
Katibu wa Itikadi na uenezi CCM Taifa Humphrey Polepole akimkabidhi ilani ya uchaguzi ya CCM 2015 - 2020 Mgombea Ubunge jimbo la Kinondoni, Ndugu Said Maulid Mtulia
Mamia ya Watu walijitokeza kwenye mkutano wa CCM katika viwanja vya Msufini kata ya Mwananyamala.

*YALIYOSEMWA NA MGOMBEA UBUNGE JIMBO LA KINONDONI KWA TIKETI YA CCM, NDUGU MAULID SAID MTULIA KWENYE MKUTANO WA KAMPENI ENEO LA MSUFINI, KATA YA MWANANYAMALA JANA ALHAMIS FEBRUARI 01, 2018*

"Nimejiunga kwenye chama chenye dola na chenye ilani ya uchaguzi, tatizo lipo wapi? - Mtulia

"Kama mimi Msaliti mbona wao wameshindwa kuungana kwa pamoja kupambana nami msaliti? Uko wapi umoja wao wa Ukawa? Nani msaliti hapo? - Mtulia

"Nyote ni mashahidi namna ambavyo nimekuwa nikitoa pesa zangu mfukoni kunyonya maji wakati wa mafuriko" - Mtulia

"Mtulia mimi nilienda Mahakamani kuzuia bomobomoa nyote mlishuhudia ubomoaji ule ulizuiwa mpaka kesho" - Mtulia

"Chama hiki ndicho kilichotoa pesa kujenga soko la Msisiri, kujenga madaraja na kujenga madarasa. Nipo kwenye chama sahihi chenye kuleta maendeleo kwa jamii." - Mtulia

"Nimekabidhiwa ilani na Polepole na nikishinda nitaanza na agizo la kuhakikisha pesa za Vijana na Wanawake toka Manispaa zinatolewa mapema iwezekanavyo" - Mtulia

"Mkimchagua Mtulia matatizo ya maji, mifereji na kuchimba mitaro, kujenga barabara na matatizo mengineyo yatakwisha kabisa" - Mtulia

"Nimejitoa mhanga ya kujiuzulu ili kuwaokoa Wana Kinondoni" - Mtulia

"Pasipo kushirikiana na Serikali mimi Mbunge ningepata wapi hela za kujenga barabara, kujenga mifereji, kujenga maghorofa? Ukiwa Kiongozi mpinzani ni ngumu kuleta maendeleo kwa Wananchi, nawaambia ukweli." Mtulia

"Nikiwa Mbunge kupitia tiketi ya CCM kutanipa urahisi wa kuwaletea maendeleo wana Kinondoni" - Mtulia

"Mkinikopesha kura zenu, nitawalipa maendeleo ya kweli wana Kinondoni. Naomba kura zenu wana Kinondoni." - Mtulia.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527