MWANDISHI WA HABARI AKAMATWA NA POLISI AKIPIGA PICHA MAHAKAMANI IRINGA


Mwandishi wa gazeti la Mwananchi mkoani Iringa, Geofrey Nyang'oro amekamatwa na polisi.
Mwandishi huyo wa habari amekamatwa na polisi wakati akiwa katika mahakama ya wilaya ya Iringa leo Alhamis Februari 15,2018.

HII HAPA TAARIFA KUTOKA KLABU YA WAANDISHI WA HABARI MKOA WA IRINGA (IPC)

Taarifa kuhusu kukamatwa Geoffrey Nyang'oro mwandishi wa Gazeti LA Mwananchi.

Mnamo majira ya SAA saba na kitu mchana akiwa katika canteen ya chakula eneo LA mahakamani Nyang'oro alikamatwa na polisi waliokuwa wamevaa kiraia kwa madai ya kupiga picha ndani ya Mahakama na kisha kupelekwa ofisi ya RCO kwa ajili ya kutoa maelezo.

Kwa mujibu wa Nyang'oro ni kwamba kabla ya mahakama kuanza alipiga picha ya mtuhumiwa Meya wa Manispaa ya Iringa Alex Kimbe kwa kutumia simu yake ya kiganjani.

Inasemeka baada ya shughuli za mahakama kuanza Hakimu alipoingia alitoa angalizo juu ya watu waliopiga picha mahakamani wakati shughuli za mahakama zikiendelea na kusambaza picha mitandaoni na kwamba yeyote anayetaka kupiga picha mahakamani in lazima yeye atoe kibali.

Baada ya mashahidi wa kesi hiyo kutoa ushahidi kesi ikaahirishwa mpaka mchana ndipo Nyan'goro akaingia canteen kula polisi wakamfuata na kumchukua.


Yaliyojiri polisi
Wamechukua maelezo yake na wamebaki na simu na kitambulisho kwa madai ya kufanya uchunguzi timemdhamini na tutarudi kesho SAA NNE kuchukua simu baada ya kujitidhidha kwamba hakupiga picha wakati shughuli za mahakama zikiendelea

Ms. Tukuswiga Mwaisumbe
KATIBU ,- IPC
15/02/2018

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527