MJADALA WA SAKATA LA MSAMAHA WA BABU SEYA WAIBUKIA BUNGENI

Mbunge wa Temeke kwa tiketi ya (CUF) Mhe. Abdalah Mtolea ameibua sakata la kusamehewa Babu Seya na mwanae, Johnson Nguza 'Papii Kocha' na kusema halikuwa jambo jema kwa kuwa watu hao mahakama iliwabaini kuwa ni wabakaji.


Mtolea amesema hayo jana Februari 7, 2018 akiwa bungeni na kudai kitendo cha watu hao kuachiwa na kupewa heshima na Serikali ikiwa pamoja na kuwapandisha kwenye majukwaa mbalimbali na kuwapa ufadhili haileti picha nzuri kwa jamii.


"Kwenye maadhimisho ya Uhuru wa Tanganyika ukatoka msamaha kwa Babu Seya na wenzake watu ambao pasipo na shaka mahakama zilithibitisha kwamba hawa watu ni wabakaji sasa tunapokuwa tunasamehe wabakaji uko wapi ulinzi wa watoto wa taifa hili,tunawapandisha kwenye majukwaa wafanye show yaani tunawaona kwamba ni kioo cha jamii je wanafundisha nini? Alihoji


Mhe. Mtolea aliendelea kusema kuwa "Je, mnataka kwamba siku ya mwisho tukiwauliza watoto ukiwa mkubwa unataka kuwa kama nani aseme nataka kuwa mbakaji?


Babu Seya na mwanaye Papii wanategemea kuachia kazi yao mpya muda si mrefu baada ya kuiaanda mara tu baada ya kupewa msamaha na Rais John Pombe Magufuli

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527