KUTANA NA NYANGUMI MUUAJI ANAYEONGEA KAMA BINADAMU

Nyangumi wa kike mwenye umri wa miaka 16

Nyangumi Muuaji anayeweza kutamka maneno kama "hello" anadhaniwa kuwa wa kwanza wa aina yake kuigiza kauli ya binadamu.

Nyangumi huyo wa jinsia ya kike alijifunza''kuzungumza" baadhi ya maneno ya binadamu kwa kunakili mwalimu wake katika eneo la hifadhi wa nyama wa baharini nchini Ufaransa.

Matamshi anayoweza kuyatamka mnyama huyo ni pamoja na jina "Amy" na "one, two, three".

Nyangumi na pomboo ni miongoni mwa wanyama wachache kando na binadamu wanaoweza kujifunza kutoa sauti za matamshi kwa kuyasikia tu.

"Katika wanyama ni nadra sana ," alisema Dkt. Josep Call wa Chuo Kikuu cha St Andrews, mtafiti mwenza katika uchunguzi.

"Ni kawaida kwa binadamu bila shaka ... la kushangaza, wanyama wanaoweza kufanya vizuri ni wanyama wa baharini."

Watafiti wanataka kubaini ikiwa nyangumi hujifunza sauti kwa kuigiza wengine. Walimfanyia uchunguzi nyangumi wa kike aliyepatiwa jina la Wikie katika sehemu ya ardhi baharini katika eneo la Antibes nchini Ufaransa.

Alifundishwa kuongea maneno ya binadamu kupitia shimo lake la kupumua na anaweza kusikilizwa kwenye sauti yake iliyorekodiwa akirudia maneno kama vile "hello" na "Amy", na kuhesabu "one, two, three", kwa sauti ya kelele ,ya kunong'oneza ama sauti laini.

Nyangumi muuaji alifahamika kuishi katika makundi yenye lafudhi za kipekee "dialects". Wanaweza kuwanakili wajumbe wengine wa aina yake nyikakani, licha ya kwamba hili linahitaji uchunguzi zaidi.Nyangumi wauaji ndani ya maji wakiwa na lafudhi za kipekee

Kwa mwanadamu ana kikomo cha matamshi katika uzungumzaji wa lugha, lakini kwa wanyama wengine ni nadra sana.

Pomboo na nyangumi wa beluga ni miongoni mwa wanyama wanaoweza kuigiza sauti kutoka kwa viumbe wengine ama wao kwa wao. Baadhi ya ndege pia wanaweza kuigiza sauti za binadamu.

Wikie alitoa sauti alipokuwa ndani ya maji huku mkia wake ukionekana juu nje ya maji. Sauti zinazotolewa chini ya maji zinaweza kuwa tofauti. Japo huyu anaweza kuwa ni nyangumi mmoja tu, watafiti hawana uhakika ikiwa kuna nyangumi wengine wanaoweza kuigiza sauti za matamshi.
Chanzo- BBC

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527